Maandalizi ya Mahakama ya Mafisadi Yaanza Jukwaa la Haki Jinai Lakutana Kufanya Tathmini

Wakati Bunge likiwa limepitisha sheria ya uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi nchini, Jukwaa la Haki Jinai ambalo linajumuisha Taasisi za umma na serikali limekutana kujipanga namna zitakavyoweza kufanya kazi kwa ufanisi kwenye Mahakama hiyo.


Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, mara baada ya kufungua kikao hicho cha kazi cha siku mbili cha jukwaa hilo.


Dk. Mwakyembe alisema jukwaa hilo limehudhuriwa na viongozi wote wa Taasisi ambazo zipo kwenye mfumo wa haki jinai ikiwemo Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Mahakama, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(Takukuru).


Alisema kikao hicho kinafanyika kipindi muafaka kwa sababu jana Bunge lilipitisha muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali ambao unatoa mwanya wa kuanzisha mahakama ya mafisadi na makosa ya rushwa.


Alibainisha vyombo hivyo vinaangalia jinsi gani kimoja kimoja kwa ushirikiano vitakavyoweza kufanikisha uanzishaji wa Mahakama hiyo.


Kikao hicho kilihudhuriwa na idara ya polisi ambayo inatakiwa ipeleleze haraka, Takukuru ifanye uchunguzi kwa haraka, Timu ya DPP na waendesha mashtaka wake wote ifanye kazi kwa ufanisi sana kesi zisikae, Mahakama nayo kama kuna vitu vinakwamisha vitatuliwe.


Alisema chombo hicho kinatafakari namna vyombo hivyo vitakavyoshirikiana ili mahakama hiyo iweze kufanya kazi kwa ufanisi kama Rais alivyoahidi.

Hata hivyo alisema pamoja na hilo wanajadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usimamiaji wa haki jinai nchini.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,Buswalo Mganga alisema changamoto zinazoikabili haki jinai nchini ni uhalifu ambao unafanywa na watanzania wenyewe na miongoni mwao wengine wanatoka nje na washirikiana na watanzania na vyombo vya habari.

Uingereza yatolewa michuano ya EURO 2016 Bofya hapa



News alert: Chile yatwaa Ubingwa tena Copa America Bofya hapa
Video: MESSI AKOSA PENATI NA KUISHUHUDIA CHILE IKITWAA UBINGWA COPA AMERICA bofya hapa 


Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa 







Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top