Meli ya mizigo yazama Bahari ya Hindi

MELI ya Mizigo ya Mv. Happy iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar imezama katika Bahari ya Hindi ikiwa imebeba mbao zaidi ya 1090 na magunia 450 ya viazi mviringo.

Hata hivyo, mabaharia 12 ambao ni wafanyakazi katika meli ya mizigo ya hiyo wamesalimika kufa maji kwa vile meli hiyo haikuzama yote katika eneo la Kizingo kisiwani Zanzibar.

Tukio hilo lilitokea jana alfajiri kisiwani Unguja. Mkuu wa Operesheni baharini, Msilimiwa Idd, alisema tukio hilo lilitokea saa 8.00 usiku baada ya meli hiyo kuyumba kutokana na dhoruba kali ya upepo.

Alisema ilipotimu saa saa 9.00usiku nahodha wa meli hiyo alipoona hali imezidi kuwa mbaya akaelekea katika Kisiwa Mchanga ambako alijikuta akikwama kwa vile upande mmoja wa meli ulikuwa unapitisha maji.


Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa 







Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top