Makumi ya maelfu ya watu wamemuaga aliyekuwa bondia shupavu Muhammad Ali nyumbani kwake katika mji wa Louisville huko Kentucky.Amir Khan
19.27pm:Bondia wa Uingereza Amir Khan ambaye alikutana na Muhammed Ali mara mbili anasema kuwa Ali alikuwa kielelezo chake.Ali alikuwa na pande nyingi lakini unapoangalia mafanikio yake katika ndondi kwa kweli ni makubwa mno,alisema.
19.18pm:Watu wamejipanga kandokando ya barabara huku msafara wa gari lililobeba mwili wa Ali ukiendelea kupita katika maeneo muhimu ya Ali wakati wa maisha yake huku baadhi ya mashabiki wake wakimsifu Ali! Ali !Mashabiki wa Muhammad Ali
19.16pm: Ibada ya mazishi itafanyka huko katika uwanja wa michezo wa Louisville
19.04pm:Muhammad Ali alikuwa hanunuliki,hauziki wale kutishwa.Ni msimamo wake ndio uliomleta karibu na wanaharakati wa haki za kibinaadamu nchini Marekani.Watu waliojitokeza kandokando ya barabara kuupa buriani msafara uliobeba mwili wa Muhammad Ali
18.32pm:Kushindwa kwa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan kuhudhuria mazishi ya Muhammad Ali licha ya kufunga safari nchini Marekani kuhudhuria kumeangaziwa na magaeti mengi ya Uturuki.
18.30pm:Kwa sasa msafara umefika katika eneo la BoulevardEneo la Boulevard
18.29pm:Maelfu ya watu wamejipanga kandokando ya barabara wakirushia maua gari lililobeba mwili wa Ali.I
Magari yaliokuwa katika msafara wa mwili wa Ali ulikuwa umeweka kipepeo
18.18pm:Kuwepo kwa maelfu ya watu katika mazishi ya Muhhamad Ali wakiwemo viongozi kutoka mataifa tofaut duniani kunaonyesha atahrai yake duniani kama shujaa.Ali alipigana katika mataifa 12 tofauti katika kipindi chake chote za masumbwi pamoja na kuhudu kama mwanaharakati wa haki za kibinaadamu.Msafara wa mwili wa Ali waondoka18.00pm:Msafara wa mwili wa Muhammad Ali watoka18.03pm:Kareem Abdul-Jabbar atoa rambirambi zake.
Ali na Kareem Abdul Jabar
Aliyekuwa gwiji wa mchezo wa mpira wa vikapu upande wa wanaume Kareem Abdul Jabar amemtaja Ali kuwa nduguye na rafiki mkubwa katika mahojiano na BBC.Amesema kwamba walijuana tangu walipokuwa vijana.Muhammad Ali ni mfano wa shujaa anayeishi .Amekuwa na ushawishi mkubwa katika vizazi na mashabiki duniani akiwa mwana michezo na mwanaharakati wa haki za kibinaadamu.katika maisha yake yote amekuwa mtu wa huruma.I
Vijana na Ali
17.15pm:Muhammed Ali alikuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa Vijana.Muhammad AliMuhammad AliMsafara wa mwili wa Muhammad Ali
17.09:pm:Gari lililobeba mwili wa Ali bado halijaondoka katika nyumba ya ibada ya mazishi lakini watu wengi wamejipanga kando kando ya barabara kuupokea na kumuaga shujaa wao.Msafara wa jeneza la marehemu Muhammad Ali utapitia njia hizi
16.05pm:Msafara huo unatarajiwa kuchukua takriban saa moja na nusuImage captionMuhammad Ali na Will Smith mmoja ya watu watakaobeba jeneza lake16.00pm:Karibu katika mazishi ya Muhammad Ali.
Umati mkubwa wa watu utachukua mwili wake na kuupitisha katika maeneo muhimu ya maisha yake kabla ya kupelekwa katika maziko.