MACHO YAKISUBIRI UTAMU WA EURO, MIGUU IKITABASAMU KULE AMERICA KUSINI

Moja kati ya vitu ambavyo nimefurahi kuvisikia katika masikio yangu ni kuhusu michuano ya Euro na Copa America. Vimekuja katika kipindi kizuri hasa sisi wapenda soka. Ukiona kile kinacho endelea kule America hakika mpira una utamu wake katika miguu ya wacheza soka wenyewe.Natamani nimwone Rooney walau
atukumbushe kitu katika kipindi chake cha upambanaji kidogo tunaweza iona Uingereza ikifanya kitu.

Kule kwa watoto wa maskini America ubora wa vipaji vyao ndiyo furaha ya macho yetu. Mboni za macho yangu tayari zinasubiri utamu wa Euro kuona namna gani ukomavu wa Marcus Rashford ukiweza kufanya kazi.

Waingereza wanaamini katika falsafa ndiyo maana mwanafalsafa wao mmoja aliwahi kusema IT IS BETTER TO FAIL IN ORIGINALITY THAN TO SUCCEED IN IMMITATION (BORA KUSINDWA KWA UHALISIA KULIKO KUSHINDA KWA KUIGA) Waingereza wanaamini hivyo kupitia miguu ya Rooney na uchanga wa Rashford katika michuano yao.

Anachoendelea kukifanya Mexico kule America anazidi tufumbua macho yetu yaliyokuwa yamefichwa na ukungu ndani yake. Wengi tunaamini ubora wa Brazil kuliko utimamu wa hawa wamexico. D. Payet walau huyu anaweza onyesha kitu na Ufaransa yake katika michuano hii ya Euro. Naiona miguu yake yenye Buggati
ndani yake, ubora wake aliokuwa nao ndani ya Barclays huenda akazidi kutupa ndani ya ardhi ya nyumbani kwao. Macho yangu yapo Euro huku miguu ikiwa kule kwa watoto wa kimaskini waliokubali kuwa soka ndiyo furaha yao.

Wakati mwingine tunatakiwa kukubaliana na mabadiliko ya tabia ya nchi walau tunaweza pata vilivyo bora kwa wachezaji wanaokuja vizuri. Cristiano Ronaldo wachache sana wasiojua ubora wake. Miguu yake imejaa kila
kitu kama mchezaji bora, sidhani kama ataweza kuendeleza makali yake ndani ya michuano hii kutokana na kutumika sana kulikomfanya wakati mwingine kucheza na sindano katika mwili wake kulikompelekea kuchoka katika game zake za mwisho.

Carrasco mmoja kati ya wachezaji wengine wanaoweza nogesha michuano hii ukimweka kando Payet katika michuano hii. Ngoja tusubiri utamu wa Euro kama utaweza kuwa na usawa na kule kwa watoto wa mitaani. Natamani kuwa karibu na dunia na kuzidi kuona kwa ukaribu michuano hii ya watoto wa mitaani na watoto
wa darasani. Imani yangu hata karamu yangu niitumiayo kuandika makala hii ingekuwa na uwezo. Muda ni wakati na ndiyo wanadamu wengi huamini hivyo.

Muda utatuambia kile kinachoendelea kule America katika michuano yao ya Copa America, wakati tutauona
ndani ya macho yetu katika michuano ya Euro inayokaribia kuanza ndani ya Ufaransa siku chache zijazo. MACHO YANGU YANAPO SUBILI UTAMU WA EURO HUKU MIGUU IKITABASAMU KWA KILE KINACHOENDELEA KULE AMERICA.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top