Euro2016 - Wales wakubali kipigo zidi ya England – Rashford akiweka rekodi


Michuano ya Euro 2016 imeendelea tena mchana wa leo kwa mchezo uliowakutanisha wana ndugu wawili kutoka katika himaya ya Malkia Elizaberth: England vs Wales.

Kabla ya mchezo wa leo, Wales ambao walikuwa wamepoteza mechi zao 4 zilizopita dhidi ya England walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda, lakini bado wameendelea kuwa wateja wa ndugu zao, baada ya kukubali kipigo cha 2-1 jioni ya leo.

Gareth Bale alianza kuifungia Wales kwa goli zuri la mkwaju wa faulo ambao ulitinga wavuni baada ya kumshinda Joe Hart dakika ya 42 ya mchezo.

Kipindi cha pili kocha Roy Hodgson akasawazisha makosa yake kwa kufanya sub nzuri ya kuwaingiza Daniel Sturridge na Jamie Vardy, ambao hawakumuangusha kocha wa baada ya kushindilia misumari miwili na kuipa England ushindi wa kwanza na muhimu katika kundi B ambal sasa wanaongoza wakiwa na pointi 4.

Kwa upande mwingine kijana Marcus Rashford ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuichezea England katika michuano ya Euro, leo aliingia dakika takribani 10 za mwisho badala ya Adam Lallana.

Uingereza sasa wamejiweka mahala pazuri wakisubiri mchezo wao wa mwisho dhidi ya Slovakia ambao jana nao walishinda kwa kuwafunga Russia ambao sasa wanashika mkia kwenye kundi lao.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top