BBC CHINESE
Ulinzi umeimarishwa nchini Hong Kong, huku Zhang Dejiang afisa wa ngazi ya juu zaidi kutoka Uchina akizuru eneo hilo, tangu maandamano ya <Endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
Polisi wapatano 6,000 wametumwa katika eneo hilo na mawe yaliyoko barabarani yameunganishwa kwa nta ili kuzuia waandamanaji kuyang’oa na kuyatumia kama silaha.
Aidha utawala wa eneo hilo umejenga ua wenye urefu wa mita mbili kuzuia umati wa watu.
Makundi kadhaa ya wanaharakati wa kijamii yamesema kuwa yanapanga kuandamana wakati wa ziara hiyo, huku baadhi yao wakipanga kuandamana hadi jengo kuu la serikali kati kati mwa mji, ambako hafla maalum ya kumlaki Bw Zhang itafanyika.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)