Mataifa 25, ikiwemo Marekani yameafikiana kuipa serikali ya Libya silaha ili kuzuia wapiganaji wa Islamic State kudhibiti taifa hilo la <Endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
Muungano huo wa kimataifa umesema utalegeza vikwazo vya ununuzi wa silaha vya Umoja wa Mataifa kuhusu Libya na kutoa misaada ya silaha na zana nyingine za kivita kwa wanajeshi watiifu kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyo na makao yake mjini Tripoli.
Waziri mkuu wa Libya, Fayez al-Sarraj, amesema kundi hilo la Islamic State ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa hilo na kanda hiyo, na kuwa msaada wa kigeni unahitajika zaidi, ikiwa utawala wa nchi hiyo unadhamira ya kufanikisha vita dhidi ya ugaidi.
Wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walikubaliana mkataba huo kwenye mazungumzo yaliyofanyika mjini Vienna,
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)