PICHA: Ajali ya Lori na Hiace Yaua Watu 9 na Kujeruhi 18


Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugonga gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Amina Masenza alisema dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace hiyo iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara.


“Lori limeharibika kabisa na Hiace pia imeharibika kabisa,” alisema Kamanda Masenza.


“Lori hilo liliposhindwa kufunga breki liliigonga Hiace ambalo lilikuwa na abiria na kwenda mbele na kisha kugonga watembea kwa miguu,,”


Kamanda Masenza alisema katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni, madereva wa magari hayo wote wamejeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi wengine.


“Dereva mmoja yupo chumba cha upasuaji kwa kuwa mguu wake umevunjika na mwingine yupo wodini,” alisema






Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top