Mchezaji wa Mbao FC afariki baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui FC




Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jana jioni baada ya kuanguka uwanjani Kaitaba wakati wa mtanange wao dhidi ya timu
ya vijana wa Mwadui FC ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.


Ismail Khalfan alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Serikali ya mjini Bukoba.


Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.


Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa katika Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.


 Habari zilizopo katika Magazeti ya leo jumatatu December 05, 2016 bofya hapa

 Mchezaji wa Mbao FC afariki baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui FC bofya hapa

Lowassa: Fidel Castro ni shujaa wangu wa dunia bofya hapa

Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo jumatatu bofya hapa 

Mzee wa Upako: Tajeni nilikunywa pombe gani na Katika Baa Gani bofya hapa 





Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top