MADHARA YA KIAPO WAKATI WA UCHUMBA..!

 

MWL Joseph b Maduka.

Kuna watu wapo katika hali ya kukata tamaa kabisa ya kuoa/kuolewa baada ya kusubiri na kuomba kwa muda mrefu bila majibu yoyote.Wakati mwingine wamefikia hali ya kusema ataoa au kuolewa na mtu yoyote Yule atakayekuja mbele yake ,maana haoni tumaini lolote katika kumsubiri Mungu.

Zipo sababu kadhaa kwanini mtu anaweza kupitia hali hiyo ,lakini leo nataka kuongelea madhara ya kiapo ambacho watu huweka wakati wa uchumba. Wengi wamefungwa hapa bila kujua ,hivyo naamini kupitia ujumbe huu utaenda kuwafungua wengi …AMINA.

Wakati wapo katika mahusiano ya awali au uchumba huwa wanafunikwa na wimbi kubwa sana la upendo ambao linawafanya hata wasiweze kuona mbele, Na ndio maana husema mapenzi ni upofu na kupitia upofu huu wengi wanaishia kujuta baadaye na kujilaumu yale waliyofanya nyuma.

Unakuta watu wapo katika uhusiano kwa malengo ya kuja kuoana hapo baadaye na wanaanza kuishi maisha ambayo kiukweli ni kama wanandoa tayari ,na mbaya zaidi wanajiingiza kwenye VIAPO kuwa hatutakuja kuachana na kama ikitokea mmoja wetu amemuacha mwenzake basi asioe /kuolewa ,wengine hudiriki hata kuweka viapo vya mauti kwa kusema kama mmoja akimuacha mwenzake basi kufa na aafe.

Bila kujua kwa maana wamefunikwa na upofu hu wa mapenzi wanajikuta wameingia kwenye mtego wa Ibilisi na kushindwa kutoka.Kiapo hiki uwa kina dumu milele kama hakitaondolewa au labda mpaka pale wahusika watakapokufa (inategemea na aina ya kiapo chenyewe).

Kuna utofauti kidogo kati Kiapo na Nadhiri,

· Kiapo ni makubaliano baina ya watu wawili au zaidi kuwa watafanya au kutofanya jambo Fulani, Na kama mmoja wao akitokea kwenda kinyume basi Adhabu Fulani itakuwa juu yake.

Watu hutumiza makubaliano hayo kwa kutaja mbingu ,kitu chochote katika dunia ,miungu au Mungu. Pia waapaji huweza kuapa kwa kutumia damu zao wenyewe kwa kuikata sehemu zao za mwili na kulishana au kuzigusanisha damu zao,huweza kutumia sadaka abayo huitoa kwa pamoja nk

Kiapo mara nyingi huusisha mtu na mtu .Soma 1 Samwei 20:12-17,Mwanzo 24 :1-4

· Nadhiri ni maombi ambayo mtu huomba kwa Mungu kwa ahadi kuwa kama Mungu akimjibu ombi lake hilo basi atafanya kitu Fulani kwa ajili ya Mungu.

Nadhiri humuusisha mtu na Mungu.Soma 1 Samweli 1 :10 -11

Sasa watu wanapoweka viapo hivyo wanaweza wakaja baadaye wakasahau ni nini ambacho wameapa na kwenda kinyume na kiapo hicho na hapo ndipo madhara yanapojitokeza,Ile adhabu waliyokubaliana kuwa itokee kama wakishindwa kutekeleza kiapo hicho hujionesha hapa na kuanza kufanya kazi.

KWANINI KIAPO KINA NGUVU

1 . IPO NGUVU KATIKA MAKUBALIANO YA PAMOJA

Neno la Mungu linasema “ Amin(Hakika) , Nawaambia yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa na mbinguni” Mathayo 18:18(a)

Hivyo kama mmeapa kuwa kama mkichana msioe/kuolewa basi mbingu itayahifadhi maneno hayo na ikitoea mmeachana duniani basi mbingu itatimiza kile amabacho mmekubaliana cha kutokuoa au kuolewa.

2 . IPO NGUVU YA UUMBAJI KATIKA KINYWA.

Binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu ( Mwanzo 1:26), mungu aliumba dunia kupitia Neno ,alitamka na vitu vikawa kama alivyotamka (Mwanzo sura 1). Hivyo kama tumeumbwa kwa mfano wa Mungu ,nguvu hiyo ya uumbaji ipo pia vinywani mwetu tunapotamka vitu (hasa kwa Imani).

Ndio maana biblia inasema “Mauti na Uzima huwa katika uwezo wa ulimi ,Na wao waupendao watakula matumda yake “ Mithali 20: 21

3 . KIAPO NI KINYUME CHA NENO LA MUNGU.

Biblia inakataza tusiape , hivo kama ukiapa utakuwa umetenda dhambi na dhabi yoyote ina hukumu.Kma ni mtu uliyeokoka halafu ukaapa ina maana utakuwa umetoka katika mapenzi ya MUngu na kumpa ibilisi nafasi ya kukutesa katika maisha yako.Na kiapo kinatesa..!

“Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa Usiape uongo ila mtimizie Bwana nyapo zako.Lakini mimi nawaambia Usiape kabisa hata kwa mbingu maana ndicho kiti cha enzi cha MUngu,wala kwa kwa nchi maana ndiyo pa kuwekea miguu yake ,wala kwa Yerusalemu kwa maana nido mji wa Mfalme mkuu , wala usiape kwa kichwa chako maana hauwezi kufanya unwele mmoja kuwa mweupe au mweusi” Mathayo 5:32-36

Kutokana na sababu hizo tulizoziona kiapo kinaweza kukutia katika mateso na kifungo kukibwa katika maisha yako na bila kufahamu hili na kupata msaada wa kiroho utaendelea kutumikia kiapo hicho na kuwa gereza lako la milele.

NIFANYE NINI ILI NIONDOKANE NA MADHARA YA KIAPO NILICHOWEKA?

· Jambo la kwanza na la muhimu ni kujichunguza ni wapi uliweka maagano na mtu na ukashinwa kuyatekeleza.

· Ingia kwenye maombi ya Toba ,tubu kwa dhambi hiyo uliyoifanya na omba Munguakusaidie kutoka hapo . Hapa wakati mwingine utahitajika hata kufanya maombi ya kufunga ya muda mrefu (Itategemea na vile Roho Mtakatifu atakavyosema nawe).

· Vunja agano hilo uliloweka kwa kinywa chako. Uliweka agano kwa kinywa chako na unatakiwa ulivunje kwa kinywa chako.

“…..Na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni “ Mathayo 18:18(b)

Fungua kiapo hicho kwa jina la Yesu.

Kama umeona unafanya hivi nabado hakuna mafanikio au Mungu anakuuongoza uende kwa mtumishi Fulani ili akusaidie basi fanya hivyo.

ANGALIZO :

USIKUBALI KUWEKA KIAPO NA MTU YOYOTE KWA AJILI YA CHOCHOTE..KIAPO CHAKO HAKIKUFANYI UONEKANE MUAMINIFU BALI KITAKUFANYA UINGIE KWENYE HUKUMU ISIYO NA SABABU.

MOYO USIKUDANGANYE ..YEREMIA 17:9

“LAKINI NFUGU ZAIDI YA YOTE NDUGU ZANGU ,MSIAPE KWA MBINGU WALA KWA NCHI ,WALA KWA KIAPO KINGINECHO..BALI NDIYO YENU NA IWE NIYO NA SIYO YENU NA IWE SIYO ,MSIJE MKAANGUKIA HUKUMU” YAKOBO 5:12

MUNGU AKUBARIKI.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top