TFF yatoa kalenda ya mwaka, Usajili wa wachezaji kuanza JUNI 15


tff
Wakati huo huo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa kalenda ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania bara kwa mwaka 2016/2017

Kalenda hiyo inaonesha kipindi kinachofuata ni usajili wa wachezaji kwa vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambapo unatarajiwa kuanza Juni 15, 2016, Usajili huo ukiaanza na uhamisho wa wachezaji Juni 15, 2016 hadi Julai 30, 2016.

Afisa Habari wa TFF Alfredy Lucas akizungumza na waandishi wa habari amesema Kalenda hiyo, kuwa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia kipindi cha Juni 15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji wa mikataba wa wachezaji.

Amesema Pingamizi za usajili zitaanza Agosti 7 hadi 14, 2016 kabla ya TFF kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, 2016
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top