SAMATTA AMEIZUNGUMZIA PENATI ALIYOKOSA DHIDI MISRI

Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta alikosa mkwaju wa penati katika mchezo kati ya Tanzania na Misri uliochezwa
jana June 4 kwenye uwanja wa taifa.

Samatta amesema penati ilikuwa ni muhimu na hakutarajia kupoteza penati hiyo lakini imetokea kwasababu ni moja ya sehemu ya mchezo.

“Sikutarajia wala sikudhani kama naweza nikakosa penati lakini ndiyo ilishatokea, ni sehemu ya mchezo. Nisingeweza kubadilisha nikauchukue mpira nje nipige tena”, alisema Samatta baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Misri.

“Tulianza mchezo vizuri, lakini baada ya wapinzani kupata goli mchezo ulibadilika kwasababu wenzetu wanajua kutumia nafasi ambazo walizipata tofauti na sisi ambao tulijitahidi kutengeneza nafasi lakini tushindwa kuwa wazuri kwenye kuzitumia”.

Samatta alisema goli la kwanza walilofunga Misri liliwavuruga wachezaji wa Stars hali iliyopelekea waruhusu goli la pili.

“Baada ya wao kupata goli la kwanza walituvuruga kwasababu hatukutegemea, muda mwingi sisi tulikuwa na mpira na tunashambulia ndiyo mchezo hauwezi kubadilisha matokeo”.

Matokeo ya mchezo wa jana yanaitupa nje Stars kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kucheza fainali za AFCON mwaka 2017 huku ikiwa imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Nigeria utakaochezwa September mwaka huu.
Credit:Dauda

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top