Ndege za kivita za Marekani
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, ameionya China kuwa Marekani inawazia kuanzisha ulinzi mkubwa wa angani kwa kubuni jeshi la anga ili kulinda maeneo ya bahari ya kusini mwa China ili kuzuia kile ambacho amesema matendo mabaya ya yenye dharau na ya kuudhi ya China.
Bwana Kerry alisema hayo alipowahutubia waandishi wa habari, pale alipofanya ziara fupi nchini Mongolia.
China, ambayo inakalia sehemu kubwa ya bahari ya kusini mwa nchi hiyo, inadai kuwa ni mali yake huku ikipuuzilia mbali vitisho vya Marekani, na kusema haitishiki kamwe.
Maeneo hayo yanang'ang'aniwa na mataifa kadhaa ya bara Asia yakiwemo Ufilipino na Vietnam.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)