Museveni amteua mkewe Janet, waziri

Museveni ataja baraza la mawaziri

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemteua mkewe Janet Museveni kuwa waziri wa elimu na michezo katika orodha mpya ya baraza la mawaziri alilotangaza.

Wizara hiyo ya elimu na michezo ni moja kati ya wizara kuu nchini humo.

Takwimu zinaonesha kuwa wizara hiyo ya Elimu na michezo hupokea idadi kubwa ya fedha za umma.

Museveni aliyeshinda hatamu yake ya tano mwezi Februari alimhifadhi waziri mkuu Ruhakana Rugunda na makamu wa rais Edward Kiwanuka Ssekandi katika orodha hiyo mpya ya baraza lake la mawaziri.Museveni amteua mkewe Janet waziri wa elimu

Aidha rais Museveni alimteua kiongozi na mpinzani wake katika uchaguzi mkuu uliopita Bi Betty Kamya, wa chama cha FDC ambaye ni waziri wa mji mkuu wa Kampala.

Uteuzi mwengine uliowashangaza wachanganuzi wa siasa ni ule wa mbunge wa upinzani bi Betty Amongi, wa chama pinzani cha UPC, ambaye sasa ndiye waziri wa Mashamba na nyumba Lands and Housing.

Museveni mwenye umri wa miaka 71 vilevile alimhifadhi Matia Kasaija na Irene Muloni kama mawaziri wa Fedha na Kawi mtawaliwa.Mpinzani mkuu Kizza Besigye alipinga uchaguzi wa Museveni akisema haukuwa wa uhuru wala wa haki.

Museveni alishinda uchaguzi mkuu uliopita na asilimia 60% za kura japo Mpinzani mkuu bwana Kizza Besigye alipinga uchaguzi huo akisema haukuwa wa uhuru wala wa haki.

Bw Besigye yuko rumande akisubiri kufunguliwa mashtaka ya uhaini baada kujiapisha mwenyewe.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top