Carneiro aafikia makubaliano na Chelsea

Eva Carneiro
Aliyekuwa daktari wa klabu ya Chelsea Eva Carneiro, ameafikia makubaliano kuhusu kutimuliwa kwake kutoka kwa klabu, nje ya mahakama.

Dr Carneiro alikuwa amepinga kutumuliwa kwake na alikuwa amchukulie hatua za kisheria meneja wa zamani Jose Mourinho.Image copyrightREUTERSImage captionJose Mourinho

Siku ya Jumatatu ilibainika kuwa Chelsea ilikuwa imempa Dr Carneiro pauni milioni 1.2 kusuluhisha swala hilo jambo ambalo alilikataa.

Chelsea ilisema kuwa inajutia kisa kilichosababisha daktari wake wa kwanza kuhama klabu hiyo.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top