Mbunge Sugu anusurika kifo, mtoto afariki kwenye ajali hiyo


Taarifa zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha ITV jana December 17 2016 zinasema kuwa mbunge wa Mbeya mjini ‘CHADEMA’, Joseph Mbilinyi amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Iyunga jijini Mbeya baada ya gari lake kufeli break na kumgonga mtoto ’15’ ambaye amefariki wakati akipelekwa hospitali.


Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa askari polisi wanne wamejeruhiwa baada ya kupata ajali wakati wakielekea kwenye ajali hiyo aliyopata mbunge Joseph Mbilinyi ‘sugu’


Gari hilo lilikuwa linaendeshwa na dereva wake, Gabriel Andrew (43) ambaye anashikiliwa na polisi.
 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top