Makada Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wazuru Tanzania Kujifunza toka CCM



UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uko nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli zinazofanywa na CCM.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama hicho, Jia Bo.


Madabida alisema lengo la ziara hiyo ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Baba wa Taifa la China, marehemu Mao Tse-Tung.


Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Temeke na Zanzibar uliwasili nchini baada ya ziara ya baadhi ya makada wa CCM waliokwenda China na kujifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.


Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.


"Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi zingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba na zinginje za Ulaya hasa katika siasa za kijamaa," alisema Chana.


Alisema China wako karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyopiga..


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top