Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Detener inmediatemente”(Simamisha hapo hapo)
Frednando alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya muongozaji wa video hiyo kusimamisha sehemu inayo muoenyesha Mercy akimkumbatia Rahab kwa furaha. Mercy akajikuta akiitumbualia macho sehemu hiyo iliyo simamishwa huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.
ENDELEA
Kila mmoja aliweza kulishuhudia tendo la Mercy kumimini kiasi cha unga unga mweupe kwenye kinywaji alicho kishika Rahab, pasipo watu wengine kuweza kumuona wakati wa sherehe hiyo kuweza kufanyika. Walio na roho nyepesi wakajikuta wakimaka kwa sauti ya juu, Mercy baada ya kuona kwamba ameweza kugundulika kwa haraka, akapandisha juu gorofani na kuingia chumbani kwake kwani anagundua kinacho kwenda kutokea ndani ya masaa machache mbeleni hakitakuwa ni kizuri kwani anautambua vizuri ukatili wa bosi wake.
Mercy akafungua kabati lake na kutoa begi dogo la mgongoni na kuanza kuingiza kiasi cha pesa alicho kuwa amekihifadho ndani ya kabati hilo kisha kwa haraka akafungua dirisha na kusimama, kabla hajafanuya chochote mlango wake ukapigwa na teke wakaingia walinzi wawili wa Frednando wakiwa na bunduki mikononi mwao
***
Hali ya Fetty na wezake, zikazzidi kushuhulikiwa na madaktari bingwa waliomo ndnai ya ngome ya bwana Rusev, komandoo wa nchi ya Rusev aliye weza kuisaliti nchi yake na kuunda kikosi chake alicho kipa jina la R.U.P.P(Rusev United Power of People). Kikundi hichi aliweza kukianzisha kwa siri kubwa tangu akiwa ndani ya jeshi pasipo watu wengine kuweza kukifahamu kwa haraka.
Akaweza kutengeneza kambi yake chini ya bahari kaskazini mwa nchi yake ya Urusi, haya yote aliweza kutafanya kwa siri kubwa akishirikia na baadhi ya viongozi wa juu serikalini walio kuwa na uchu mkubwa wa madaraka. Mbaya zaidi ni kwamba viongozi hao walitaka kumgeuka, ila kwa kutumia umahiri wake aliweza kuwaangamiza kwa mkono wake mwenyewe kuhakikisha kwamba siri yake haiwezi kuvuja kwa mtu wa ina yoyote kwamba yeye anamiliki jeshi kubwa la vijana kinyume na sheria za nchi yake..
R.U.P.P, ikazidi kukua miaka kwa miaka na kuzidi kupata wataalamu wakubwa wa mitambo na kuanza kutengeneza silaha za nyuklia kisiri sana.
Ndani ya miaka ishirini ya usiri, siku moja bwana Rusev aliweza kuja kujikuta siri yake ya kuwa ni muasi ndani ya nchi yake ikagundulika, hii ni baada ya siku hiyo kunywa kiasi kikubwa sana cha pombe na kujikuta akilala ma malaya mmoja aliye weza kumpa penzi tamu, hadi akajikuta akianza kumuambia mambo yake ya ndani huku akimuahidi kumpa nafasi ya kuweza kufanya naye kazi.
Binti huyo pasipo kuwa mvumilivu akajikuta akijinadi kwa rafiki zake, juu ya kupata nafasi ya kuajiriwa na bwana Rusev katika kikosi chake cha siri cha R.U.P.P, hii ni mara baada ya binti huyo kutoka kulala na bwana Rusev ambaye kwa kipindi hicho bado alikuwa ndani ya jeshi la nchi ya Rusia.
Bwana rusev hakuwa na jinsi zaidi ya kuamua kuiasi nchi yake mara baada ya serikali kuanza kumfwatilia na kumuwekea vikwazo vingia hadi kutaka kumuhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ila haikuwa ni rahisi kwa serikali, kwnai watu wa bwana Rusev waliweza kumtorosha kiongozi wao huyo walio muabudu kama Mungu wao, na kuweza kumuweka katika mazingira salama ambayo ni ngumu sana kwa mtu yoyote kuweza kumfikia na kumdhuru.
“Jamani tupo wapi?”
Anna alikuwa wa kwanza kuzungumza mara baada ya kuzinduka kutoka usingizini. Akashangaa eneo zima la chumba kikubwa walicho lazwa na kilicho tawaliwa na rangi nyeupe kwenye kuta zake kuanzia chini, pembeni hadi juu. Akawatazama wezake na kuwakuta bado wakiwa wamejilaza kitandani, huku wakiwa na madripu ya maji. Anna akajitazama na yeye na kujikuta akiwa na dripu kwenye mkono wake wa kushoto, nguo walizo kuwa wamezivaa mara ya mwisho hawakujikuta nazo, alijishuhudia akiwa amevishwa mavazi meupe yanayo fanana na wezake.
Baada ya muda kila mmoja akazinduka na wote wanne wakajikuta wakipiwa katika hali ya kuto fahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea katika eneo walilo kumbuka.
“Jamani hapa tulipo tunaonekana kila kona”
Fetty alizungumza baada ya kuzitazama kamera za ulinzi zilizo kuwa katika kona nne za chumba walichomo.
“Sasa kamani tutafanyaje, kwa mana hapa mimi sielewi?”
Halima aliuliza akiendelea kuyapepesa macho yake
“Kikubwa tuweni wapole, kwa maana kama hawa watu wangekuwa ni wabaya kwetu wanegesha tuu, ila wemeweza kutuhudumia hadi hapa”
Fetty aliwasisitiza wezake, kabla Agnes hajazungumza, bwana Rusev akaingia huku akiwa ameongozana na walinzi wake wawili pamoja na daktari mmoja, mwenye umri mkubwa kiasi.
“Munaendeleaje mabinti”
Bwana Rusev alizungumza kiswahili fasaha kilicho wafanya wote wanne kushangaa na kumtumbilia macho kwani siku zote walikuwa wanajua kwamba mzee huyo atambui kishwahili
“Munanishangaa mimi kuzungumza kishwahili? Ok tuachane na hayo, kama munavyo weza kujionea mupo katika mikono salama sana, na kwaupande mwingine pia si salama”
Fetty na wezake wakatazama kwa macho yakujiiuliza ni kwanini Bwana Rusev anasema sehemu hiyo ni salama ama si Salama, hapakuwa na aliye kuwa na jibu la kuzungumza kwa mwenzake zaidi ya kukaa kimya kusubiri ni kitu gani ambacho bwana Rusev atazungumza.
“Natambua kwamba nyinyi ni miongoni mwa mabinti mahiri mulio weza kufanya matukio kadhaa kwenye nchi ya Tanzania, na pia hadi sasa hivi bado munaendelea kutafutwa si ndio?”
Anna akajibu kwa kutingisha kichwa akikubali kwamba ni kweli bado wanatafutwa
“Sawa sasa ni hivi, nawapa uchaguzi wa haya nitakayo kwenda kuyazungumza. Kwanza mukikubali kuwa na mimi nitawapa nafasi kubwa ya kuyatambua mambo mengi ambayo hamjawahi kuyajua. Pili mukikataa kuwa na mimi miili yenu itakuwa ni chakula cha papa walio zunguka eneo hili.”
“Wakati ni wenu kukubali au kukataa”
Bwana Rusev alizungumza na kutoka nje ya chumba hicho. Ukimya ukatawala ndani ya chumba huku kila mmoja akiwa na maswali mengi kichwani mwake.
“Jamani mimi nipo tayari”
Halima alizungumza huku akinyanyuka kwenye kitanda alicho kaa na kusimama wima, wezake wote watatu wakamkodolea mimacho wakimshanga
“Musinishangae bwana, hivi munahisi kuna mtu anaye weza kutoka hapa, ni bora kuwa wapole na hii siku nyingine tujifunze kukurupuka kama angekuwa si yule mwehu Samson, leo tusinge kuwa hapa”
Halima alizungumza kwa kujiamini, huku jazba ikianza kumpanda taratibu, Anna naye taratibu akasimama wima na kupiga hatua hadi sehemu alipo simama Halima
“Hata mimi nimekubali”
Fetty na Agnes wakatazamana kwa macho ya kunto fahamu, nafsini mwao kila mmoja alijihisi kuwaona Halima na Anna kuwa ni wadhaifu na kujirahisisha na kuwa watumwa wa bwana Rusev.
“Kwa nini munafanya hivyo”
Fetty aliuliza kwa sauti ya chini, iliyo jaa majonzi kiasi
“Tumeamua kuwa wapole kama ulivyo tusisitiza, hatuna njia nyingine zaidi ya hii”
Halima alijibu huku akimkazia macho Fetty ambaye kwa muda wote amekuwa kama kiongozi wao, ila kwa sasa hawakuhitaji kusikiliza amri ya mtu yoyote zaidi ya kuamua kufwata akili zao. Agnes akanyanyuka taratibu na kusogea walipo simama Halima na Anna. Fetty akabaki peke yake kitandani huku akiwashangaa wezake. Kwa upole Agnes akanyoosha mkono wake wa kulia na kumuomba Fetty kuwa pamoja na nao.
Fetty akainamisha kichwa cheke chini, huku akijifikiria kwa mara kadhaa, akaunyanyua uso wake ulio jaa machozi yaliyo tapakaa usoni mwake, kwa kasi akanyanyuka na kukumbatiana na wezake huku akiendelea kumwagikwa na macho mengi.
“Sisi ni timu moja, hata kama tupo chini ya mtu tusiachene”
Agnes alizungumza huku mkono wake mmoja ukimpiga piga Fetty mgongoni.
***
Mercy akatazamana kwa muda na askari walio ingia chumbani kwake wakihitaji kuweza kumkamata na kumpelekea mbele ya bosi wake ambaye kwa muda huu amefura kwa hasira kali. Miguu na mwili mzima vikaanza kumtingishika kwa muda, askari mmoja akapiga hatua za haraka kwenda dirishani alipo simama, kabla hata hajamfikia, Mercy akaamua kujirusha kutoka juu gorofani na kwabahati mbaya, akageuka hewani, na kichwa chake kikatangulia chini na kutua kwenye sakafu ngumu iliyopo nje, na hapo hapo Mercy akapoteza maisha.
Ripoti ya Mercy kujiachia gorofani ikamfikia Frednando, kwa haraka akatoka nje akiwa na walinzi wake pamoja na wafanyakazi wengine waliio kuwa wakimsubiria Mercy kuletwa sebleni, kwani yeye ndio muhusika aliye weka madawa ya kulevya kwenye kinywaji cha Rahab.
Hakuna aliye weza kuamini kuweza kumkuta binti mzuri kama Mercy akiwa amepoteza maisha yake kwa jambo ambalo wote walipelekea kuliwaza kwamba ni vivu wamapenzi
“Mtoeni, apelekwe hospitalini kuhifadhiwa”
Frednanando alizungumza kwa lugha ya kimexco, kisha akandoka huku akijifuta jasho jingi lililo kuwa likimwagika usoni.
***
Gafla Rahab akazifumbua macho, na kuanza kuyapepesa kila upande wa chumba alichopo, akakutana na sura ngeni, kwa haraka akawatambua watu hao kwamba ni madaktari, kwani mavazi yao meupe na marefu kiasi yalikuwa ni kielelezo tosha kwa wao kuweza kujulikana
“Nipo wapi hapa”
Rahab alizungumza kwa sauti ya kukwaruza kiasi, nesi akaagizwa na daktari kuweza kwenda kumuita Raisi Praygod Makuya
“Unaitwa”
Nesi alizungumza kwa lugha ya kingereza, Raisi Praygod kwa haraka akanyanyuka katika sehemu aliyo kuwa amekaa na kwenda katika chumba alicho mke wake, kitendo cha kuingia macho yake akayatupia kitandani na kumkuta mke wake akiwa ameketi huku akiwa katika wasi wasi mwingi. Raisi Praygod akamsogelea Rahab na kumkumbatia kwa nguvu huku machozi yakimwagika.
“Praygod nipo salama mume wangu?”
“Kweli?”
“Ndio mume wangu, najisikia vizuri”
Madaktari wote ndani ya chumba wakabaki wakiwa wamemshangaa Rahab kwani utafiti wao unaonyesha amepewa sumu kali sana ila chakushangaza mngonjwa amestuka na kuwa mzima kama si yeye aliye letwa akiwa katika hali mbaya.
“Hapa kuna kitu kinacho endelea, si rahisi akaamka kama hivi”
Daktari mmoja alimnong’oneza mwenzake kwa lugha ya kispain, huku wote macho yao wakiwa wamemtama Rahab anaye tabasamu huku akimkumbatia mume wake.
SHE IS MY WIFE(38)
Madaktari wakaomba nafasi ya kuweza kumpima tena, Rahab kuhakikisha kwamba yupo salama kama anavyo dai, Praygod hakuwa mbisha zaidi ya kusogea pembeni huku akiwa na furaha kubwa sana moyoni mwake kwani mke wake kwa sasa yupo katika hali ya usalama. Wakamchoma Rahab sindano kwenye mkono wa kushoto, wakatoa damu kiasi na kuiweka kwenye chupa, kisha madkatari wawili wakelekea kwenye chumba cha maabara ili kuanza kuifanyia uchunguzi damu ya Rahab
“Mume wangu mbona una wasiwasi mwingi kiasi hicho?”
Rahab aliuliza kwa sauti ya mahaba iliyo jaa unyonge ndani yake
“Nilikuwa na wasiwasi mwingi mke wangu nilihisi kama nimekukosa wakati bado ninakuhitaji”
“Usijali mume wangu mimi nipo salama”
Rahab alizungumza huku akiachia tabasamu pana usoni mwake.
Madaktari walio chukua damu ya Rahab na kuipia wakajikuta wakipatwa na wasiwasi mwingine ambao, mmoja wao Alisha hisi kwamba kuna kitu ambacho kinaendelea na nitofauti sana na walivyo hisi. Walicho kiona ni virusi ambao hawakujau hata wamatokea wapi kwani ni wadogo wadogo na wanazunguka kila kona ya damu. Uchunguzi ukazidi kuendelea huku wakijaribu kutafuta dawa ambayo inaweza kuua virusi hao waliopo kwenye mwili wa Rahab.
“Jamani, tumejaribu kila aina ya dawa kuwaangamiza hawa virusi ila hawajafa”
Doktari mmoja alizungumza baada ya kumaliza majaribio yote katika kutafuta dawa ya kuangamiza virusi hao.
“Jamani nimepata wazo”
“Wazo gani?”
“Hembu tuchukue kiasi kidogo cha hii damu kisha, tuiingize kwa mbwa, ili kuweza kutambua kwamba je vinamadhara au laa”
Wazo la daktari huyo wa kike halikuweza kupingwa, kwa haraka wakatafuta mbwa, kisha wakamchunguza hana magonjwa yoyote, walipo ridhika, wakachukua damu kidogo ya Rahab na kuichoma kwa mbwa huyo kisha wakamfungia kwenye moja ya chumba ambacho kimezungukwa na vioo na nirahisi kwao kuweza kumuona mbwa huyo na endapo atakuwa na mabadiliko ya aina yoyote basi itakuwa ni rahisi kwao kuweza kugundua madhara ya mbwa huyo.
Frednando akafanikiwa kufika hospitalini huku, akiwa katika hali ya furaha baada ya kusikia kwamba mke wa rafiki yake amzinduka kutoka katika hali ngumu na mbaya aliyo kuwa nayo. Frednando hakuamini kumkuta Rahab akiwa anazungumza huku anacheka kwa furaha kama alivyo weza kumuona akiwa katika furaha hiyo masaa mengi yaliyo pita kwenye arusi yao.
“Imekuaje kaka?”
“Yaani hata mimi sifahamu kaka, mimi nahisi ni miujiza ya Mungu kwa maana ikutegea kama mke wangu atazinduka”
“Aisee shemeji pole sana”
“Asante shemeji yangu”
Furaha ikarudi upya kwa watu hao watatu, ila Frednando hakuzungumza chochote kuhusiana na jinsi Mercy alivyo husika katika kutaka kumuu Rahab, kwani tayari muhusika amejiangamiza yeye mwenyewe.
“Ila madaktari wamechukua damu ya mke wangu wanaifanyia uchunguzi, kwani nao hawakuamini kama ataweza kuamka muda huu”
“Mmmm……!!”
“Ndio tunasubiria waweze kutupa majibu”
“Sawa, amekula lakini?”
“Hapana shem, nipo vizuri tu”
Rahab alizungumza kwa furaha ambayo Frednando na Raisi Praygod wakabaki wakiwa wametazamana, kisha wakaaungana na Rahab kuachia tabasamu.
Mbwa aliye wekewa damu ya Rahab akaanza kutokwa na puvu jingi mdomoni mwake, huku akirusha rusha miguu, baada ya hapo akatulia sakafuni tuli, jambo lililo wafanya madaktari kuzidi kuchanganyikiwa kwani mbwa huyo tayari amesha fariki. Kila mmojaa akabaki kimya akiwa amemkodolea mbwa huyo macho, wasiwasi mwingi ukaanza kuwavaa kila mmoja kwani kila mmoja alianza kupatwa nahisia mbaya dhidi ya Rahab.
“Jamani oneni kule”
Daktari mmoja alizungumza huku akikinyooshea kidole chake shemu alipo lala mbwa, aliye anza kujitingisha mguu mmoja, baada ya hapo mbwa huyo akanyanyuka na kukaa sawa, kama alivyo kuwa hapo awali
“Jamani ni nini hichi?”
Daktari mwengine aliuliza kwani kila linalo tokea hapo ni muujiza kwao kwani mbwa huyo waliamini kwamba amesha aga dunia. Wakiwa katika kushangaa shangaa, mlango wa maabara ukafunguliwa na Rahab akaingia na kusimama katikati ya mlango huo, huku macho yake akiwa amewakazia madaktari hao walio anza kutetemeka kwa woga.
***
Fetty na wezake baada ya kukubaliana kuungana na bwana Rusev wakaanza kutembezwa katika vitengo mbali mbali ndani ya ngome hii, iliyopo chini ya bahari. Hapo ndipo wakagunduka kwamba wapo chini ya bahari na ningumu sana kwa wao kuweza kutoka katika eneo hilo lenye vifaa vingi ya ulinzi ikiwemo kamera na askari wanao linda kila kona kwa masaa ishirini na nne.
Fetty akajikuta akivutiwa sana katika kitengo cha watu wanao tengeneza silaha za nyuklia, bwana Rusev baada ya kuligundua hilo akaamuru Fetty kuweza kufundishwa mara moja jinsi ya kutengeneza silaha hizo ambazo wanazitengeneza kwa wingi katika eneo hilo.
Halima na Anna wakajikuta wakipenda kuendesha ndege za kivita ambazo zimo ndani ya eneo hilo. Bila kinyongo bwana Rusev akahitaji mabinti hao kuweza kuwa kaatika kundi hilo. Agnes, kwa umahiri wa kulenga shabaha kwa kutumia bunduki, akajikuta akiingia katika kikosi cha subshotter, watu wanao lenga shabaha kwa masafa marefu. Ubora wa Agnes uliweza kuwapita watu wote walio kuwemo katika eneo hilo, jambo lilizo kumpa sifa nyingi Agnes.
Kuingia kwa mabinti hao wanne ndani ya kngome ya bwana Rusev, kukaleta mabadiliko yaliyo makubwa sana, kila mmoja akajikuta akiwa anafanya kazi kwa juhudi ili wasiweze kupitwa na mabinti hao ambao mara nyingi bwana Rusev aliweza kuwamwagia sifa kwamba ni mahiri sana katika kazi zao. Kitu kingine kilicho zidi kuwapa sifa Fetty na wezake ni jinsi uwezo wao wa kupigana pasipo kutumia silaha, ulivyo mkubwa, hadi wakaanza kuwa ni tishio kwa wababe waliomo ndani ya kambi hiyo.
“Kuna kazi”
Bwana Rusev alizungumza baada ya kuwaita Fetty na wezake ndani ya ofisi yake, mara baada ya kuridhika na jinsi wasichana hao walivyo weza kufanya juhudi katika mafunzo yao.
“Kazi gani?”
Agens aliuliza huku akiwa amemtazama bwana Rusev machoni mwake
“Kazi nyenyewe inakuhusu sana wewe, Agnes, baada ya wiki mbili waziri wa mambo ya nje nchini Marekana atakuja hapa Russia na atafikizia kwenye jiji la Mossow.”
Bwana Rusev akameza mate kidogo kisha akanedelea kuzungumza
“Lengo lake kubwa kuja katika nchi hii, anahitaji kuweza kuingia makubaliano na serili yetu kuweza kusaidiana nao katika swala zima la kuzuia sila za nyuklia zisitengenezwe duniani kote”
“Picha zake zipo?”
Fetty aliuliza
“Ndio zipo”
Bwana Rusev akaminya kitufe kidogo kilichopo kwenye meza yake, chumba kizima kikawa na giza jingi, mwanga wa Tv kubwa iliyomo ndani ya chumba hicho ikawaka, bwana Rusev akanyanyuka na kuisogelea kwenye ukuta ilipo wekwa. Akaanza kuminya minya kwenye kioo cha Tv hiyo, na picha za waziri huyo zikatoke.
“Kwa jina anaitwa bwana Paul Henry Jr. Ni miongoni mwa viongozi ambao wanalindwa sana katika dunia hii, ukiachilia Raisi wao na makamu wake, huyu ndio anafwatia kwa kulindwa sana”
“Atakuja tarehe 22 ya mwezi huu, ataongozana na walinzi zaidi ya mia moja. Watakao mzingira katika msafara wake watakuwa zaidi ya thelathini”
“Hili ndio njengo ambalo atafikia, ni hotel ya kitalii na iliyo anza kuwekewa ulinzi kuanzia sasa hadi hapo atakapo kuja”
Bwana Rusev aliendelea kutoa maelezo ya Hotel atakayo fikizia bwana Paul Henry Jr, akaonyesha kila sehemu ambayo bwana Paul Hery Jr atapita akiwa na watu wake wanao mlinda. Hadi mwisho wa maelekezo yake, wote wakawa wamemuelewa vizuri bwana Rusev.
“Agnes hii ni kazi yako ya kwanza na sinto hitaji ukosee, ninakuamini sana”
“Usijali mkuu nipo kwa ajili yako”
“NITAHITAJI UMUUE KIONGOZI HUYU IWE TISHIO KWA NCHI HII NA DUNIA NZIMA”
“SAWA MKUU”
Agnes alijibu huku akiinamisha kichwa chake chini kama ishara ya kumuheshimu bwana Rusev, kisha bwana Rusev akachuku moja ya chini yenye alama ya X na kumvisha Agnes shingoni, akampa Baraka kwa ajili ya kuitekeleza kazi hiyo hatari sana kwa maisha yake.
==> ITAENDELEA
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 33 & 34 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 29 & 30 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 27 & 28 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 15 & 16 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 13 & 14 bofa hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 11 & 12 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 9 & 10 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 27 & 28 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 15 & 16 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 13 & 14 bofa hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 11 & 12 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 9 & 10 bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)