Godbless Lema Afikishwa Mahakamani Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana

Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema leo amefikishwa mahakamani mkoani Arusha na kusomewa shtaka la uchochezi kwa viongozi wa serikali.


Lema amefikishwa jana mahakamani akiwa tayari amekaa rumande takribani siku 7 tangu alipokamatwa.


Lema anakabiliwa na shtaka la uchochezi ambapo ni pamoja na kumtishia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kauli yake aliyoitoa dhidi ya Rais Dkt Magufuli kuwa Mungu amemuonyesha asipojirekebisha atafariki.


Baada ya kusomewa shtaka hilo, Lema amerejeshwa rumande baada ya kukosa dhamana kufuatia pingamizi lililowekwa na upande wa Jamhuri.


Mahakama imeeleza kuwa itatoa uamuzi kuhusu dhamana ya Lema Novemba 11 mwaka huu.

 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top