Siku chache baada ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kipilimuka, Wilaya ya Nzega mkoa Tabora, Jackson Sanga kuchapwa viboko na baadhi ya wakazi kwa kutowapigia makofi sungusungu, Mwalimu Zephani Kapelele wa shule hiyo amejikuta katikati ya uwanja wa mpira usiku wa manane.
Pia, walimu wengine 11 wameandikiwa barua za kutishiwa kuuawa.
Akizungumzia mkasa huo, Mwalimu Kapelele alisema tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kumuona nyoka jikoni kwake waliyefanikiwa kumuua na kumtupa.
Mwalimu Kapelele alisema walipoingia kulala aliota ndoto ya ajabu, baadaye alijikuta akiwa kwenye uwanja wa shule hiyo hadi wanafunzi na walimu walipomkuta asubuhi.
Diwani wa Kata ya Mwantundu, Pascal Nicolaus alisema mwalimu huyo walimkuta akiwa amelala katikati ya uwanja huku wanafunzi wakiwa wamemzunguka.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)