Papa Francis amtunuku Mtanzania

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amemtunuku tuzo ya heshima ya mfano mwema Mtanzania, Janeth Mhella kutokana na utumishi uliotukuka.
Mhella amekuwa Mwafrika wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo na Papa Francis, kutokana na kumtumikia vyema kiongozi huyo na kanisa kupitia kazi aliyoifanya kwenye kituo cha redio.


Taarifa iliyochapishwa jana na gazeti dada la The Citizen, ilieleza tuzo hiyo ya juu na ambayo mtu hawezi kuipata kwa urahisi ilitolewa Alhamisi iliyopita na Kiongozi wa Sekretarieti ya Mawasiliano ya Ofisi ya Papa, Monsinyori Dario Vigno. Pia, watumishi wengine watano walitunukiwa tuzo na sekretarieti hiyo.


Tuzo hiyo kwa Kiitaliano inaitwa ‘Pro Ecclesia et Pontifice’ yaani medali ya Latini na kwa Kiswahili fasaha ni medali ya kanisa na Papa. Tuzo hiyo ya Kanisa Katoliki ilianzishwa na Papa Leo wa 13 mwaka 1888.




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top