Mmoja wa watafiti waliouawa Chamwino mkoani Dodoma, Teddy Lumanga ni mjane ambaye aliomba safari hiyo ili apate fedha za ada ya mtoto wake anayetarajia kujiunga chuo.
Lumanga aliuawa na wenzake wawili katika mauaji ya kinyama yaliyofanywa na wananchi wa Kijiji cha Iringa-Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma, kwa hofu watafiti hao walikuwa mumiani.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kituo cha Utafiti wa Udongo cha Selian kilichipo mkoani Arusha, Benjamin Mkumbo alisema Lumanga aliomba mwenyewe kuwamo katika safari hiyo kwa lengo la kupata fedha za kuhudumia watoto wake.
Alisema, Lumanga alikuwa mjane aliyekuwa na jukumu la kuwalea watoto wake wawili baada ya kufiwa na mumewe ambaye naye alikuwa mtumishi wa kituo hicho.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)