JUMUIYA za Vijana wa Chama cha Wananchi ( CUF) katika mkoa wa Dar es Salaam, wameibuka na kulaani tabia ya inayojiita Kamati ya Uongozi ya chama hicho inayoongozwa na Julius Mtatiro, kutoa lugha za kubeza dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
, Jaji Francis Mutungi.
, Jaji Francis Mutungi.
Vijana hao wamedai hatua hiyo ya Mtatiro na wenzake, kutumia vyombo vya habari hasa redio na televisheni, kumkashifu Msajili wa vyama kwa maamuzi yake ya kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho kwa mujibu wa katiba, haikubaliki.
Viongozi wa vijana wa chama hicho katika wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni, wakizungumza na waandishi wa habari jana, walimtaka Mtatiro kuacha kuwakashifu viongozi hao vinginevyo wataomba uongozi kuwachukulia hatua kulingana na Katiba ya chama ikiwemo kuondolewa uanachama.
Akisoma taarifa ya upotoshaji unaofanywa na wanaojiita Kamati ya Uongozi wa chama hicho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa chama hicho wilaya ya Ilala, Canal Shughuly, alisema Katiba ya chana hicho inaamini kwamba kila mtu ana wajibu wa kuheshimu utu, uhuru na haki za wengine pamoja na kutii sheria halali za nchi.
Shughuly aliongozana na Katibu wa Vijana wa chama hicho Ilala, Abdul Komesha na Katibu wa Kinondoni, Yusuph Kitogota alisema kitendo cha kubezwa kwa msajili pamoja na maamuzi yake wakati anatambulika kikatiba ni kuonesha jinsi alivyo mbumbumbu wa kuielewa katiba ya chama anachokiamini.
Alisema Mtatiro ni miongoni mwa vijana waliopata bahati ya kushika nafasi ya juu ya uongozi wa ndani ya CUF ya Naibu Katibu Mkuu bara ambayo aliteuliwa na Lipumba, lakini uteuzi huo ulitenguliwa baada ya kukubwa na kashfa ya ubadhirifu wa Sh milioni 86 kwa ajili ya ununuzi wa bendera na vifaa vingine vya chama.
Akijibu tuhuma hizo, Mtatiro alidai vijana hao waliozungumza si viongozi wa chama hicho. Alisema wakati wa uongozi wake kama Naibu Katibu Mkuu Bara, ndipo kwa mara ya kwanza chama hicho kilianza kupata hati safi toka kwa msajili wa vyama na hakuwahi kuwa na tuhuma zozote.
Alisema anachofanya katika vyombo vya habari ni kutoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ya chama hicho, huku akikanusha taarifa za kuwa mgogoro uliopo ni baina ya bara na visiwani.
“Nitaendelea kukusema linalomhusu yeyote anapofanya jambo siyo sahihi na kama ni ubadhirifu uliofanyika ndani ya chama ni kwa Lipumba kuchukua zaidi ya bilioni 280 kwa wabunge mwaka jana akidai kugombea urais,” alisema.
PICHA 5: Tingatinga Lilivyofukua mamilioni yaliyokuwa Yamefichwa ardhini bofya hapa
Waziri atolea maelezo taarifa ya serikali kuhakiki watumishi wanavyotumia mishahara yao bofya hapa
Waziri atolea maelezo taarifa ya serikali kuhakiki watumishi wanavyotumia mishahara yao bofya hapa
TCRA yakipa onyo kali kituo cha runinga cha Clouds, Yakifungia kwa miezi 3 kipindi cha 'Take One' kwa kukiuka kanuni za utangazaji. bofya hapa
Polisi Aliyerekodiwa Akipokea Rushwa Kuchukuliwa Hatua bofya hapa
Jeshi La Polisi Nchini Latoa Onyo Kali Kwa Wananchi Wanaojichukulia Sheria Mkononi. bofya hapa
Tanzania na Congo DRC zimesaini mkataba wa makubaliano kutafuta mafuta Ziwa Tanganyika bofya hapa
Mambo Muhimu Waliyoyajadili Rais Magufuli na Rais wa Congo DRC Joseph Kabila wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Polisi Aliyerekodiwa Akipokea Rushwa Kuchukuliwa Hatua bofya hapa
Jeshi La Polisi Nchini Latoa Onyo Kali Kwa Wananchi Wanaojichukulia Sheria Mkononi. bofya hapa
Tanzania na Congo DRC zimesaini mkataba wa makubaliano kutafuta mafuta Ziwa Tanganyika bofya hapa
Mambo Muhimu Waliyoyajadili Rais Magufuli na Rais wa Congo DRC Joseph Kabila wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)