Utafiti wa maambukizi mapya ya VVU waja


 Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na shirika lisilo la kiserikali la Marekani la ICAP, ina mpango wa kufanya utafiti ili kubaini watu wenye maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi (VVU) na kujua
maendeleo ya wanaotumia dawa za kufubaza virusi hivyo (ARV).



Akizungumza na wataalamu wa afya wa wilaya za Mkoa wa Manyara mjini hapa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa ICAP, Mihayo Bupamba amesema watatumia mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma kufanya utafiti huo.





Bupamba amesema wanalenga kufanya utafiti kwa kaya 16,000 nchi nzima ili kuangalia namna ya kuwasaidia waathirika na wanakusudia kutoa elimu kwa wanaotumia ARV.





Amesema hadi sasa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika Bara la Afrika wamefikia milioni 25.8 na hiyo ni idadi kubwa kwa nchi zinazoendelea.



Bupamba amesema lengo lingine la utafiti huo ni kuisaidia Serikali isiendelee kupoteza nguvu kazi ya Taifa. “Wapo watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na wanaendelea vizuri na kazi za ujenzi wa Taifa kwa kuzingatia masharti ya madaktari na sisi ICAP tumeona ni vizuri kuendelea kutoa elimu kupitia utafiti huo, ”amesema.



Ameongeza kuwa: “Tunataka kufahamu uelewa wa wananchi juu ya ugonjwa huu na kupata maoni ya wahusika na utafiti huu utahusisha rika zote bila kubagua na kwa mara ya kwanza hata watoto ambao hawajawahi kushirikishwa watapimwa”.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top