Mbaroni kwa kunyonga mkewe


Mkazi wa Kijiji cha Igate, Kata ya Nzera wilayani Geita anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumnyonga mkewe Dotto Frederick (25) baada ya kuibuka
ugomvi kati yao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema kuwa mauaji hayo yalitokea nyumbani kwa mtuhumiwa.


Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Oktoba Mosi eneo la Machimboni Kijiji cha Muranda Kata ya Buseresere wilayani hapa baada ya kuishi mafichoni kwa siku 15.


Kamanda Mwabulambo amesema mtuhumiwa huyo alimnyonga mkewe kwa kutumia kipande cha nguo na mwili wake kuuficha uvunguni.


Amesema taarifa za kiintelejensia ndizo zilizofanikisha kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.


Mwambulambo amesema wamemsafirisha mtuhumiwa huyo kutoka wilayani Chato kwenda Geita kwa mahojiano kabla ya kupandishwa kizimbani kusomewa shtaka la mauaji.


Katika tukio lingine, mwili wa mkazi wa Lugeye wilayani Magu mkoani Mwanza, Isaya Magembe (32) umeopolewa ndani ya Ziwa Victoria baada ya kuzama wakati akivua samaki na mwenzake.


Kamanda Mwabulambo amesema tukio hilo lilitokea Septemba 28 mwaka huu katika Kitongoji cha Chato Beach.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top