Trump achukizwa na matumizi mabaya ya kodi nchini Marekani

Donald Trump,mgombea urais kupitia chama cha Republican

Mgombea urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump ambaye amekuwa katika shinikizo la kutoa taarifa zake za ulipaji kodi. Trump amejiganya kuwa ni mtiifu wa sheria za kodi na kusema kuwa amekuwa akilipa kodi hata kama ni dogo.

Donald Trump aliwaambia hayo wafuasi wake wakati akiwa katika jimbo la Pueblo lililopo Colorado na kudai kuwa lilikuwa jukumu lake yeye kama mfanyabiashara kutumia vipengele vya sheria za kodi ili aweze kunufaika nazo yeye mwenyewe, wawekezaji na wafanyakazi wake. Hivyo anachukizwa sana jinsi anavyoona jinsi Marekani inavyotumia kodi.Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic

Kwa upande wake, mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Hillary Clinton aliwaambia wafuasi wake wakati akihutubia mkutano wa hadhara huko Akron,Ohio kwamba Trump anataka kutumia vibaya baadhi ya vipengele vya sheria za kodi na kuongeza kuwa Trump aliwahi kuwaangusha au kutowasaidia wafanyabiashara wadogo pamoja na kuwaacha njia panda wafanyakazi wake.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top