TFDA ‘yawamwagia sumu’ wajasiriamali

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imesema haitakubali nyumba wanazoishi watu zitumike kama viwanda vya kusindika bidhaa.


Meneja Elimu kwa Umma na Huduma kwa Wateja wa TFDA, James Ndege alisema hayo alipoulizwa na gazeti hili kuhusu malalamiko ya wajasiriamali wanaoshiriki maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogovidogo (Sido) jijini hapa na kumalizika jana.


Awali, katika risala yao, wajasiriamali hao walilalamikia TFDA na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), wakidai mamlaka hizo zinaweka masharti mengi yanayokwamisha usajili na kupata leseni za ubora wa bidhaa wanazotengeneza.


Pia, walilalamikia ugumu wa kupata vibali kutoka TFDA na kwamba, hata leseni zina masharti magumu na gharama zake zipo juu.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top