Vielelezo viwili na mashahidi 13 wa upande wa mashtaka vimeiwezesha Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, kuwahukumu vifo wakazi watatu wa Kijiji cha Mbala, Wilaya ya Chunya mkoani hapa.
Kutokana na ushahidi huo, Mahakama hiyo iliwahukumu watu hao kunyongwa hadi kufa baada ya kuwaua kwa makusudi wakazi wenzao watatu.
Washtakiwa hao ni Apolinari Mateo (30), Barnaba Siwinga (38) na Michael Claud (24), ambao kwa pamoja walipatikana na hatia ya kuwaua Julius Mwamasonga, Sabela Boniface na Maongezi Mkusi waliokuwa wakiishi kijijini hapo.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Dk Adam Mambi alisema Mahakama imeridhishwa na ushahidi huo uliotolewa na upande na walalamikaji pasipo kuacha shaka kuwa, washtakiwa walitenda kosa hilo.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)