IPTL yawaangukia wananchi

Kampuni ya kufua umeme ya IPTL imeamua kukata rufaa kwa wananchi kupinga uamuzi uliotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID), wa kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuilipa Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong Sh320 bilioni na riba ya asilimia nne.


Kampuni hiyo imewasilisha kwa wananchi hoja 14 za kupinga hukumu hiyo, ikiwa ni pamoja na kutetea malipo yenye utata ya Sh306 bilioni ya fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow yaliyoingiiza nchi kwenye mjadala mkubwa uliosababisha mawaziri na vigogo wengine kujiuzulu.


Katika hukumu hiyo iliyotolewa na ICSID Septemba 12, Tanesco imetakiwa kuilipa Standard Chartered fedha hizo, ikiwa ni malipo ya tozo ya uwekezaji na riba, fedha ambazo benki hiyo ilipinga zisilipwe kwa IPTL mwaka 2014, lakini zikalipwa katika hali ambayo ilionekana kuwa na utata mkubwa.


“Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan Africa Power Solutions (T) Limited (PAP) zimepokea kwa masikitiko habari zilizochapishwa na vyombo tofauti kuwa, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeshindwa katika vita ya muda mrefu ya kisheria dhidi ya Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCBHK),” inasema taarifa ya kampuni iliyotolewa kama tangazo gazetini.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top