Neno la Kichuya kwa mashabiki wa Simba




Kichuya amefunga goli lake la kwanza kwenye mchezo wa watani wa jadi tangu asajiliwe Simba kwenye dirisha la usajili lililopita, huu ni msimu wake wa kwanza akivalia jezi nyekundu katika michezo ya ligi
kuu Tanzania bara.

Baada ya kupiga kona iliyozama moja kwa moja wavuni, amesema mechi ilikuwa ngumu lakini anashukuru timu yake angalau imepata pointi moja.

“Nashukuru Mungu kwasababu tulikuwa tunatafuta pointi, mimi nimefunga goli ili kuisaidia timu yangu lakini si kupata sifa, lengo lilikuwa kupata pointi tatu lakini Mungu katujaalia tumepata pointi moja tunashukuru”, alisema mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Kichuya amesema mechi ilikuwa ngumu lakini kitu anachoshiru ni kumalizika salama kwa mchezo huo uliokuwa na presha kubwa.

“Mechi ilikuwa ngumu lakini nashukuru mchezo umemalizika salama.”

Mechi za Simba na Yanga huwa zinapresha yake, kwa upande wa Kichuya yeye amese hivi: “Mechi ilikuwa ni ya kawaida tu kama mechi nyingine.”

Nikamwambia atoe neno kwa mashabiki wake na Simba kwa ujumla baada ya kumalizika kwa mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka la Bongo.

“Wakae wasubiri mambo mengi yanakuja kutoka kwenye timu yao ya sasahivi.”

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top