Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema azua tafrani kwenye uzinduzi wa hospitali ya mama na mtoto jijini Arusha




Picha ikionyesha kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akitulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza katika uzinduzi huo
wa pili ni kutoka kulia ni mfadhili wa Mradi huo ambeye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na mtoto duniani Dk.Edru Broun.



Mwananchi aliyehudhuria katika uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye hakupenda kutaja jina lake akimuomba mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa hutuba.

MKUU wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemumbua mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema wakati wa uzinduzi wa hosptali ya mama na mtoto katika eneo la Bruka lililopo wilayani Arumeru .

Gambo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa hosptali hiyo aliishukuru kampuni ya mawakili ya Mawala (Mawala Advocate )kwa kutoa eneo hilo kwa ajili ya hosptali hiyo ambayo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi ya Martenity Africa.

Mara baada ya Rc. Gambo kutoa kauli hiyo Lema alisimama na kuanza kupiga kelele akidai kuwa kiwanja hicho amekitafuta yeye jambo ambalo siyo kweli kwani kiwanja hicho kilitolewa na kampuni hiyo ya uwakili.

Hata hivyo Rc. Gambo alilisitiza kuwa eneo hilo awali lilikuwa mali ya kampuni ya uwakili ya mawala ambayo ilitoa eneo hilo kwa ajili ya kujenga hosptali ya kutoa huduma kwa mama na mtoto.

“Kwa niaba ya serikali naishukuru sana kampuni ya mawala ambayo imetoa eneo hili kwa ajili ya ujenzi wa hosptali hii ambayo ina umuhimu mkubwa”

Akizindua ujenzi huo ambapo alikuwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti Gambo aliwahakikishia wafadhili hao kuwa serikali iko pamoja nao katika ujenzi wa hosptali hiyo ili kuwezesha kutoa huduma bora kwa wanannchi.

Ukweli huo ulionekana kumkera Lema na kuonekana kuwa ameumbuka na kudai kuwa ardhi hiyo ameitafuta yeye jambao ambalo lilipuuzwa na uzinduzi ukaendelea kama kawaida.

Kwa upande wake mwenyekiti wa taasisi ya Martenity Africa Mchungaji Prf. Wilfred Lau alisema taasisi hiyo imekusudia kujenga hosptali hiyo lengo likiwa ni kusadia mama na mtoto haswa tatizo la Fistula linalowakumba kina mama wengi wajawazito.

Kwa mujibu Prf. Lau alisema mradi huo kwa hatua ya kwanza utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni mbili.

“Mradi huu awamu ya kwanza utagharimu dola za kimarekani milioni mbili na ukikamilika tutatoa elimu kwa wakunga jinsi ya kuwakinga kina mama wajawazito na ugonjwa wa fistula”. Alisema hosptali hiyo itakoa maisha ya kinamama wengi kutoka maeneo ya vijijini kutokana na wakunga katika maeneo hayo kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya kudhibiti ugonjwa huo wa Fistula

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top