Katibu Mkuu wa Chadema atoa kauli nzito kufuatia tafrani kati ya Lema na RC wa Arusha tafrani kwenye uzinduzi wa hospitali ya mama na mtoto jijini Arusha


Nimesikitishwa sana na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuvuruga sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya huduma za mama
na mtoto.

Si tu kwamba ameonyesha kukosa staha kwenye jamii, pia ameonyesha kutounga mkono mahitaji ya nchi na dunia nzima "hasa kwa mahitaji ya akina mama na watoto"

Nalaani tabia hizi za kihuni zisizo na tija kwa Taifa. Ikumbukwe tu kwamba; mwanzo wa ngoma ni lele. Tabia ya Mkuu huyu wa mkoa inajenga chuki na yaweza kuleta machafuko yasiyo ya lazima. Mtu wa hivi hafai kabisa katika jamii

Tumpinge!
Katibu Mkuu Chadema Dr Vicent Mashinji.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top