DC Hanang’ awageuzia kibao wachungaji


Ikithibitika kuwa wamekuwa wakiwapotosha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii Iliyoboreshwa (iCGF), huenda wachungaji wilayani hapa wakajikuta wakikabiliwa na mkono wa dola.


Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara, Sara Msafiri alitoa onyo kwa baadhi ya wachungaji kuwa atawachukulia hatua kali za kisheria wanaowapotosha wananchi kuhusiana na iCHF.


Hatua hiyo ilijitokeza kutokana na baadhi yao kudaiwa kuwaambia waumini wao wasichangie fedha kwenye mfuko huo kwani wanapaswa kujiwekea akiba mbinguni na siyo duniani.


Msafiri ametoa agizo hilo akiwa kwenye uzinduzi wa mfuko huo kwenye Tarafa ya Simbay, baada ya mmoja wa wananchi wa eneo hilo kulalamikia kitendo cha baadhi ya wachungaji kukwamisha juhudi hizo.


Amesema wananchi wanapaswa kujiunga kwa wingi kwenye mfuko huo kwa kuchangia Sh30,000 ili wapate matibabu kwa mwaka mzima kwa kaya yenye watu na siyo kusikiliza maagizo potofu ya wachungaji hao.


“Hata kama mgonjwa mwenye iCHF ndiyo amefika muda huo na kumkuta mtu mwenye fedha zake amepanga foleni, inabidi huyu wa kadi apishwe ili akapate huduma, hivyo wananchi jiungeni kwa wingi na mfuko huu,” amesema.


Mhudumu wa Afya wa Kijiji cha Masusu, Elizabeth Darema aliwalalamikia baadhi ya wachungaji wa eneo hilo kutumia vibaya majukwa ya imani kukwamisha juhudi za watu kujiunga na iCHF.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, George Bajuta alisema watawafuatilia suala hilo ili kumaliza tatizo hilo.



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano October 12, 2016 bofya hapa


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top