Azam, Yanga, zimeshindwa kutamba uwanja wa Uhuru



Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Azam FC ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Yanga umeshuhudiwa ukimalizika bila timu hizo kufungana.

Mchezo huo ulikuwa ni wa saba kwa upande tisa kwa upande wa Azam wakati kwa Yanga ni mchezo wa nane. Yanga imeongeza idai ya michezo ambayo wametoka sare na kufikisha mechi tatu ambazo wametoka sare huku wakiwa wamepoteza mchezo mmoja wakati na kushinda mechi nne Azam nao wametoka sare katika mechi tatu wamefungwa tatu na kushinda tatu.



Yanga ilipata ushindi wake wa mwisho kwenye mchezo wa Jumatano iliyopita kwa kuifunga Mtibwa Sugar goli 3-0 wakati Azam ushindi wao wa mwisho ulikuwa September 10, 2016 walipoifunga Mbeya City 2-1 uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 15 sawa na Mtibwa Sugar pamoja na Kagera Sugar lakini zikitofautiana nafasi kutokana na magoli ya kufunga na kufungwa wakati Azam wenyewe wapo nafasi ya saba kwa pointi zao 12 baada ya mechi 9



Mtukio
Juma Abdul alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kulazimika kupumzishwa baada ya kuumizwa na Daniel Amoah dakika za mapema kipindi cha kwanza kisha nafasi yake ikachukuliwa na Mbuyu Twite.
Kipindi cha pili Yanga ilipata pigo jingine kufuatia beki wake wa kati Andrew Vicent ‘Dante’ kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na mkongwe Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Matokeo

Ruvu 1-0 Mbeya City

Mtibwa Sugar 0-0 Tanzania Prisons

Toto Africans 1-2 Majimaji FC

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top