Audio: Baada ya Yanga kutangaza kukodishwa, Baraza la Michezo Tanzania limetoa maamuzi haya…

Mohamed Kiganja-Katibu Baraza la Michezo Tanzania


Siku moja baada ya klabu ya Yanga kuweka hadharani mkataba wake wa ukodishwaji wa klabu hiyo kwa kampuni inayojulikana kwa jina la Yanga yetu Limited, Baraza la Michezo Tanzanzani (BMT) limevitaka
vilabu vya soka nchini Tanzania hususan Simba na Yanga kufuata sheria na taratibu sahihi kabla ya kufanya mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji .

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema, Baraza la Michezo linatambua kuwa vilabu vinavyotaka kufanya mabadiliko vina malengo ya kupata mafanikio na kama baraza linabariki mafanikio hayo lakini lazima taratibu za zifuatwe ikiwa ni pamoja na wanachama wao kupata fursa ya kujadili jambo linalotaka kutokea kwenye klabu yao pamoja na kupata ufafanuzi pale inapobidi sambamba na kupatiwa elimu pale inapobidi juu ya faida na hasara za mifumo husika.

Klambu za Simba na Yanga zipo katika mchakato wa kufanya mabadiliko huku Kiganjaakisisitiza ni lazima sheria na taratibu zifuatwe ili kutawapa mamlaka ya kufanya mabadiliko hayo.





Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi October 08, 2016 bofya hapa








Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top