Filamu ya CUF yaongeza washiriki

Bodi ya Wadhamini wa CUF, imetangaza kutomtambua Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na kupinga mambo saba anayofanya ikiwamo kuteua bodi nyingine.


Mwenyekiti wa bodi hiyo, Abdallah Said Khatau alisema hayo jana katika ofisi za makao ya chama hicho, Vuga, Zanzibar kuwa wamechukua hatua hiyo kwa kutambua wajibu wao kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya CUF.


Khatau alisema bodi yake imepuuza uamuzi wa juzi wa Profesa Lipumba kumteua Thomas Malima kuitisha kikao cha Bodi ya Wadhamini.


“Lipumba kwa sasa si mwenyekiti tena wa CUF na pia si mwanachama baada ya kufukuzwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa,” alisema.


Alisema bodi hiyo itaendelea kuwajibika kwa Baraza Kuu la Uongozi Taifa kama inavyotakiwa na ibara ya 98(5) ya katiba ya chama na itaheshimu uamuzi wote wa Baraza hilo.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top