Yanga yaichapa Simba kipigo cha mbwa uwanja wa Taifa



Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amesema jezi ya Donald Ngoma imemsaidia kufunga magoli mawili kwasababu ukivaa jezi ya mkali lazima na wewe uwe mkali, hiyo ni baada ya kuisaidia timu ya Wabunge wa Yanga kupata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Wabunge wa Simba .



Nchemba alifunga magoli mawili kati ya matano katika mchezo kati ya wabunge wanaoshabikia Yanga dhidi ya wale mashabiki wa Simba mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa taifa.



Magoli mengine ya Wabunge wa Yanga yalifungwa na Jadal Hamisi dakika ya 4, Musa Sima dakika ya 5 na Hamidu Bolali dakika ya 9 na kukamilisha bao tano katika mchezo huo.



“Timu zilijiandaa lakini Yanga tulisikiliza vizuri maelekezo ya waali wetu Mwamoto na Hafidh Ally na timu yetu ilikuwa composed imecheza kwa kuelewana na tulimtanguliza Mungu ndiyo maana mambo yetu yalikuwa mepesi”, alisema Nchemba baada ya mechi kumalizika.



“Wenzetu tulikuwa tunakuja nao vizuri lakini walipofika Ocean Road wakapaki pembeni wakaanza kuvunja mayai na nazi huku wakichota maji ya baharini, mpira wa kisasa hautegemei tunguli kwahiyo waliharibu saikolojia yao ndio maana tukawafunga mapema.”



“Nimevaa namba ya mkali Donald Ngoma, ukivaa namba ya mkali na wewe lazima uitendee haki na nimeitendea haki, hii ni ishara kwamba tarehe 1 October atakuwepo Ngoma mwenyewe uwanjani.”



Mechi hiyo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwasaidia wahanga waliokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.



Katika mchezo mwingine, Bongo Movies walishinda kwa mikwaju ya penati 5-4 kufuatia sare ya kufungana goli 1-1 kwenye dakika 90.


Video Mpya : Diamond Platnumz ft. Rayvanny - Salome bofya hapa





Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top