Waziri Mkuu wa Uingereza aliyejiuzulu, David Cameron amejiuzulu ubunge


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amejiuzulu nafasi yake ya ubunge na kupisha uchaguzi mdogo katika jimbo lake la Witney.

Cameron ambaye alijiuzulu nafasi yake ya Waziri Mkuu wa Uingereza Juni mwaka huu baada ya kupigwa kwa kura ya Uingereza kujitoa ndani ya Muungano wa Ulaya (EU) amesema kuwa hatiki kuwa kikwazo kwa Waziri Mkuu wa sasa, Theresa May.

Cameron amekuwa Mbunge wajimbo la Witney tangu mwaka 2001. Alisema kuwa ni furaha kubwa kulitumikia jimbo hilo kwa miaka yote hiyo lakini itakuwa ni vigumu kwake kuendela kuwa mbunge bila kuwa kikwazo katika shughuli serikali.

Aidha, alieleza kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo alimuelewa pindi alipomwambia kuhusu uamuzi huo wa kujiuzulu.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top