Breaking News: Rais wa zamani wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi afariki dunia

 
ALIYEKUWA rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kati ya tarehe 7 Aprili 1972 hadi 30 Januari 1984, Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia mchana wa leo nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Saalam
baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kimethibitishwa na mmoja wa wanafamilia ya marehemu.


 
Marehemu Jumbe atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuiongoza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar akichukua nafasi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu Abeid Aman Karume aliyefariki mwaka 1972.
(Ujumbe wa Zitto Kabwe kufuatia kifo Rais Mstaafu wa Zanzibar bofya hapa) 

Enzi za uhai wake akiwa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar alishirikiana na rais wa wakati huo wa Tanzania na mwenyekiti wa chama cha TANU marehemu Julius Nyerere kuanzisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvunja vyama vya TANU na ASP na kuunda chama kimoja cha CCM. 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top