ISSA MAEDA HAUNGI MKONO SAMATTA KUITWA STARS V NIGERIA

 
Baada ya klabu ya Genk kutoa tahadhari kwa TFF kumfanyia vipimo Mbwana Samatta kabla ya kucheza mechi ya kimataifa dhidi ya Nigeria, mchambuzi wa masuala ya michezo kutoka Clouds Media Group Issa Maeda amesema haoni kama kulikuwa na ulazima wa Samatta kuitwa kwenye kikosi cha Stars kitakachocheza dhidi ya The Super Eagles.

Maeda amesema ni vyema Samatta angeachwa apumzike na badala yake nafasi yake ingeenda kwa kijana mwingine kwa ajili ya kujenga uzoefu kwa vijana wengine kwa ajili ya siku zijazo.

“Mimi sioni sababu ya Samatta kuitwa kwenye michezo kama hii kwasababu hatugombei kitu chochote kwanini aje? Kunawachezaji wengi vijana ambao wameonekana katika ligi na kama mwalimu alikuwa makini kuangalia michezo michache ya ligi kuu atakuwa aliona vijana waliofanya vizuri baada ya raundi mbili za ligi”, alisema Maeda kwenye kipindi cha Sports Extra cha Cloud FM.

“Angeweza kuwaita hao na kuwapa uzoefu kwa ajili ya kupata akina Samatta wengine, leo Samatta yupo fit anaitwa timu ya taifa je, kama asingekuwa fit, ni nani angechukua nafasi yake? “

“Sidhani kama Nigeria wataita kikosi chao cha wachezaji waliozoeleka kucheza kila siku, nadhani watakuwa wamewaita baadhi ya vija waliokuwepo kwenye ile timu ya Olympic na wengine ambao hawana uzoefu wa kucheza timu ya taifa kwasababu hakuna wanachogombea pia.”

“Kocha angechukua baadhi ya vijana kutoka timu ya Serengeti Boys waingie kwenye kikosi cha taifa wakachezepengine wangefanya vizuri kuliko kushindwa kuwaamini huku tukimwamini Samatta kumbe tunaendelea kumuumiza.”

“Mchezaji kama Theo Walcott, wakati anacheza timu ya taifa ya England alikuwa na miaka 16 lakini alikuwa naaminiwa na akaonesha anauwezo wa kufanya vizuri siku za baadaye. Wayne Rooney, Jack Wilshare ni wachezaji ambao walipewa nafasi kwenye timu ya taifa wakiwa na umri mdogo.”

“Kwahiyo ni vizuri hata kwa vijana wa Serengeni Boys wangepewa nafasi ya kusafiri na timu kwenda Nigeria kwasabababu hata kusafiri na timu pia kunatoa uzoefu.”
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top