Ufaransa na Uingereza lawamani kwa kuangusha utawala wa Gaddafi Libya

Uingereza na Ufaransa zilitekeleza mashambulio ya kutoka angani dhidi ya wanajeshi wa Gaddafi


Ripoti ya kamati ya bunge nchini Uingereza imekosoa hatua ya Uingereza na Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kuondolewa mamlakani kwa Kanali
Muammar Gaddafi nchini Libya mwaka 2011.

Kamati hiyo ya Mambo ya Nje imesema Uingereza iliongeza chumvi ilipokuwa inaeleza hatari ambazo zingewakumba raia baada ya serikali ya Gaddafi kuanza kukabiliana na maasi.

Mpango wa kuingia kati kusaidia mwishowe ulitumiwa kama fursa ya kubadilisha utawala, ripoti hiyo inasema.

Inamtuhumu aliyekuwa waziri mkuu David Cameron kwa kukosa kuandaa mkakati mahsusi kuhusu Libya.

Wabunge hao wanasema hilo lilisababisha kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mzozo wa wahamiaji, ukiukwaji wa haki za kibinadamu na kukua kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wanaojiita Islamic State Afrika kaskazini.Nicolas Sarkozy na David Cameron waliongoza kampeni dhidi ya Gaddafi

Msemaji wa serikali ya Uingereza ametetea serikali na kusema muungano wa mataifa ya Kiarabu, Arab League, pamoja na Umoja wa Mataifa, wote waliunga mkono hatua hiyo ya kijeshi.

Gaddafi aliuawa na waasi 20 Oktoba, 2011.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top