Uamuzi wa Serikali juu ya watu wanaofanya mauaji kwa kigezo cha kutetea haki za wakulima na wafugaji


Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amesema kwamba, Serikali iko tayari kuwaachia wafungwa wengi zaidi chini ya mpango wa parole ili kuyafanya magereza yaweze kupata nafasi ya kuweka wafungwa ambao watapatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya mauaji kwa kigezo cha kutetea haki za wakulima na wafugaji.

Waziri Nchemba aliyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule (Profesa J) aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya dola wanaojihusisha na mauaji ya wakulima na wafugaji huku vyombo vya dola vikishindwa kuwachukulia hatua.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top