Tambwe aipania Stand


Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe
 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Amissi Tambwe ametamba kuwa mfungaji bora huku akiahidi kufunga mabao wakati Yanga leo itakaposhuka dimbani kucheza na Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Tambwe msimu uliopita alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 21 kwa sasa ana mabao matatu sawa na mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo baada ya kucheza michezo minne ya ligi.

Akizungumza na gazeti hili Tambwe alisema kutokana na ushindani uliopo atajitahidi kuhakikisha anatumia kila nafasi kufunga ili kujihakikishia kutetea tuzo hiyo ambayo mpaka sasa amechukua mara mbili akiwa na timu za Simba na Yanga.

“Ushindani umeongezeka sana, hivyo nitatumia kila nafasi nitakayoipata uwanjani kufunga ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuandika historia ya kuchukua ufungaji bora kwa mara pili mfululizo nikiwa na timu yangu hii ya Yanga,” alisema Tambwe.

Tambwe ambaye yupo mkoani Shinyanga na timu yake anatarajiwa kuwepo kwenye kikosi kitakachocheza na Stand United leo ambapo amepania kucheka na nyavu kila atakapopata nafasi. Kombinesheni ya mshambuliaji Donald Ngoma imezidi kuwa nzuri ambapo msimu uliopita ndiyo ilikuwa kombinesheni iliyozalisha mabao mengi katika ligi nzima.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top