Stand United yaiduwaza Yanga




Stand United ‘Chama la Wana’ wamevunja rekodi ya Yanga baada ya kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Bao pekee la Stand limefungwa na Pastore Athanasi ambalo limeifanya timu take iibuke na pointi tatu kwenye uwanja wa nyumbani.



Licha ya Stand kuwa kwenye mpasuko mkubwa wa kiutawala, timu hiyo bado haijapoteza mchezo wowote hadi sasa tangu kuanza kwa ligi mzimu huu 2016-2017.

Stand United meshinda mechi tatu na kutoka sare kwenye michezo mitatu. (Stand UTD 0-0 Mbao FC, Kagera Sugar 0-0 Stand UTD, Stand UTD 1-0 Toto Africans, Mwadui FC 2-2 Stand UTD, Stand UTD 2-1 Ruvu JKT, Stand UTD 1-0 Yanga)

Rekodi za Yanga zilizo vunjwa na Stand United
Stand United imeifunga Yanga kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ya Shinyanga mjini ilipopanda daraja.
Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza wa VPL msimu baada ya kucheza mechi nne bila kufungwa. Mara ya mwisho Yanga kupoteza mechi ilikuwa 3-1 dhidi ya TP Mazembe nchini DR Congo katika mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya makundi.
Stand United imekuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga. Awali Yanga ilikuwa imecheza mechi nne za ligi bila kuruhusu goli huku yenyewe ikiwa imefunga magoli nane. (Yanga 3-0 African Lyon, Ndanda 0-0 Yanga, Yanga 3-0 Maji Maji, Mwadui 0-2 Yanga).



Matokeo ya leo yanaifanya Stand UTD ifikishe jumla ya pointi 12 na kukaa nafasi ya pili nyuma ya Simba SC inayoongoza ligi ikiwa na pointi 16, Yanga inashuka chini kwa nafasi moja hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 10 sawa na Azam FC lakini Yanga yenyewe imecheza mechi 5 huku ikiwa na mechi moja mkononi.



Mechi inayofuta kwa Yanga itakua dhidi ya Simba wakati Stand United itasafiri hadi Songea kucheza dhidi ya Maji Maji ambayo inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa haijapata hata pointi moja baada ya kucheza mechi sita za VPL.






Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top