Simba, Yanga mwendo wa kimya kimya



 Siku moja kabla ya watani wa jadi, Yanga na Simba kuvaana katika mechi ambayo joto lake tayari limepanda zaidi kwa mashabiki na wapenzi wa klabu
hizo, maandalizi ya vikosi vya timu hizo kuelekea mchezo huo yanafanywa kimya kimya.

Mbali ya ukimya huo, pia usiri umetawala maandalizi ya timu hizo zilizoko kisiwani Pemba na mjini Morogoro kwa siku kadhaa sasa.


Tofauti na miaka ya nyuma ambako tambo, mbwembwe nyingi zikiwamo za viongozi waandamizi wa timu hizo vilikuwa vitu vya kawaida, safari hii hali imebadilika.


Mwanzoni mwa wiki, timu hizo ziliingia kambini, Yanga ikitokea Shinyanga, ambako ilicheza Jumapili na kufungwa na Stand United bao 1-0 na Simba iliyokuwa Dar es Salaam kwa mechi dhidi ya Majimaji ya Songea Jumamosi iliyopita kushinda mabao 4-0.


Timu hizo ziliondoka kimya kimya Dar es Salaam, Simba ikitangulia usiku baada ya mchezo huo dhidi ya Majimaji na Yanga ilitua Pemba, Jumatatu asubuhi kwa ndege ya kukodi.


Wachezaji wa timu hizo ambao kwa kawaida huwa wazungumzaji, wamezuiwa kusema kupitia vyombo vya habari, uamuzi unaotajwa kuwa na lengo la kutowavuruga kisaikolojia kabla ya dakika 90 za mchezo huo.






Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top