Korti yatupa kesi dhidi ya Pierre Nkurunziza



Rais wa Burundi,Pierre Nkurunzinza 

Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na taasisi tatu za kiraia kupinga uhalali wa Pierre Nkurunziza kugombea urais
kwa kipindi cha tatu mfululizo.
Taasisi hizo zilikuwa zinadai kuwa katiba ya Burundi inazuia mtu kuongoza nchi kwa vipindi vitatu.


Jaji wa mahakama hiyo, Isack Lenaola amesema walalamikaji katika kesi hiyo, Jukwaa la Asasi za Vyama vya Kiraia vya Nchi za Afrika Mashariki (EACSOF), Chama cha Wanasheria wa Afrika (Palu) na Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) walifungua kesi hiyo nje ya muda.


Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Katibu Mkuu wa EAC, Tume ya Uchaguzi ya Burundi (Ceni) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Burundi.


Hata hivyo, Jaji alisema Ceni iliondolewa kutokana na kutokuwa na sifa ya kushtakiwa katika mahakama hiyo.
 Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa September 30 bofya hapa




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top