Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.
Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea
Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea
Tukuyu kikazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari
laWaziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na
wote walitoka salama katika ajali hiyo.
Alisema baada ya kupata ajali walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
ambapo walifanya uchunguzi kubaini kama wameumia au laa! Lakini bahati
nzuri Daktari aliyewafanya uchunguzi alisema hawakuumia
Alisema baada ya hapo Waziri na wenzake waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge
Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.
Askari wa usalama barabaran wilayani Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea
Picha zote kwa hisani ya Mbeya yetu
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)