
Sababu za kuahirishwa kwa mchezo huo zinaelezwa kuwa ni uwanja kujaa maji kupitiliza kufuatia mvua kubwa iliyoambana na radi kubwa yenye mwanga mkali kunyesha uwanjani hapo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Man City, kuahirishwa huko kunatokana na sababu za kiusalama
Tiketi zilizokatwa kwaajili ya mchezo huo uliopaswa kufanyika usiku wa kuamkia leo bado ni halali.
Hata hivyo, taarifa zaidi zinaeleza kuwa Monchengladbach walitaka mchezo wao uchezwe saa 2:00 za usiku lakini Man City wamedai hakutakuwa na ulinzi wa kutosha.
Upande mmoja wa goli katika uwanja huo ndiyo ulionekana kuharibiwa zaidi na maji. Mvua hiyo imesababisha hadi hitilafu kwenye mfumo wa kielectroniki
Mwamuzi Bjorn Kuipers wa wenzake waliufanyia uchunguzi uwanja majira ya saa 2:55 za usiku lakini baadaye baada ya dakika 30 wakatoa taarifa ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)