EVERTON YAMCHANGIA MILIONI MIA 6 SHABIKI WA SUNDERLAND

Bradley Lowery (aliyebebwa kulia) amealikwa na Everton kwenye uwanja wa Goodson Park wakati wa mchezo wa marudiano dhidi ya Sunderland

Everton yaiahidi milioni mia 6 (Paundi 200,000) familia ya mtoto mwenye miaka mitano, shabiki wa Sundeland, ili kusaidia matibabu yake ya kansa nchini Marekani.

Wachangishaji wamepanga kukusanya Paundi 700,000 zaidi ya Bilioni 2 za Kitanzania ili kumsaidia Bradley Lowery, ambaye alikuwa moja ya watoto wanaosindikiza wachezaji pindi waingiapo uwanjani (ma-escot) katika mchezo wa juzi ambao Sunderland walifungwa 3-0 na Everton, uwanjani kwao, Stadium of Light.

Klabu hiyo ya Merseyside imetoa mchango huo mkubwa baada ya kujua kuhusu ugonjwa huo unaomkabili Bradley.

Klabu hiyo iliandika katika ukurasa wake wa Twitter: “Tunamtakia Bradley kila la kheri, upendo na sapoti yote ya watu wote wa Everton iko pamoja naye.

“Klabu itamualika Bradley na familia yake kwenye mechi ya marudiano, Goodison Park, na jezi zilizosainiwa na wachezaji katika mechi ya leo usiku (juzi usiku) zitauzwa katika mnada ili kusaidia mfuko.”

Mashabiki katika mechi ya jana waliimba jina la Bradley pale dakika ya tano ya mchezo ilipofika, huku wengine wakishika mabango yaliyoandikwa “Tuko pamoja nawe, Bradley” kuzunguka uwanja.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top