KWA NINI WANAUME WANAVUNJA UAMINIFU WA NDOA (kuchepuka)


Na Mwl Joseph b Maduka

Wanaume wanawindwa sana na malaya:

1⃣ Kwa kuwekewa mitego - Mithali 7:10.."mavazi ya kikahaba.."
Wanavaa nguo za nusu uchi ili wanaume waone watamani.
Udhaifu mkubwa wa mwanaume uko kwenye macho, akiona; Mathayo 5:27, Ayubu 31:1.
Mfalme Daudi,alimwona mwanamke akioga, akatamani na akazini.
1 Samwel 11:1-13.

2⃣ Kuna Wanawake Wanaotaka kupata watoto..Isaya4:1.."wanawake saba wanamtafuta mwanamume mmoja.."
Wanataka mtu watakayezaa naye.
Hasa kama hajaolewa, au ni mjane, au ameachika au mume wake hawezi kutunga mimba. Ezekiel 16:32.

Hata kwa wanaume wanaotafuta watoto nje ya ndoa kama Ibrahimu kwa Hajiri- Mwanzo 16:4-6.

3⃣ Wanaume wanapenda wanawake wanaopatikana "available.." na wanaowajali hisia zao na kuwatosheleza
Mitha. 7:13 " ...akambusu.."
Wako wanawake wazito sana kuwabusu waume zao.
Ila hapo unaona wawindaji, wanakutana na mume wa mtu wanambusu chapuchapu na kumkumbatia...Mith.5:19-20.
Kama hajafanyiwa hivyo muda mrefu na wake zao, wanachanganyikiwa, bila neema ya Mungu anajiendea ....Mithali.7:21-23

4⃣ Wanaume wanawindwa na wanawake wanaotaka hela zao.(kuchuna buzi)
Mithali 29:3
"..Ashikamanaye na makahaba hutapanya mali.."
Wanaume wengi wamekuwa mawindo, kwa sababu wana hela, na wanawake wanaozitaka ni vigumu wazipate bila kuwapata kimapenzi.

Na wanawake wengine hutumia hata nguvu za kichawi kunasa wanaume, ambao wanakuwa wagumu kupatikana. Ezekiel 13:18,20.

5⃣ Wanaume kunyimwa tendo la ndoa kwa muda mrefu. 1 Korintho 7:5 "msinyimane....mkajiane tena; shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. (Kukaa muda mrefu bila kufanya tendo la ndoa)
Mwanamume (adult) kwa siku mwili wake unazalisha mbegu za kiume nyingi sana (zaidi ya milioni mia moja) na zinahifadhiwa kwa muda.
Na zikimjaa zinamsumbua na kutaka kutoka.
Akikosa Neema anawinda nje ndoa.
Ni muhimu sana mwanamke kuhakikisha anachukua risasi zote kwa mumewe, angalau mara mbili au tatu kwa wiki.
Vinginevyo amwombee sana, maombi ya ulinzi na kumfunika kwa Damu ya Yesu. Hosea 2:6-7.

6⃣ Kuwepo kwa mazingira ya ukaribu; kwa kuwa pamoja kwa muda mrefu au kwa kumhudumia mfano, kazini, safarini na hata nyumbani na house girl (Mithali 7:18-21)

Anayekujali na kukuhudumia anapata nafasi moyoni mwako.
Na mtu anayeupata moyo wako, anaweza kuupata mwili kwa urahisi- MOYO NI CHEMCHEMI. Mithali 4:23.

7⃣ Mwanamke anayeongea maneno mazuri, malaini na matamu. Mithali 2:16; 5:3; 7:21.
Na sio maneno ya ugomvi na uchokozi. Mithali 21:9, 19; 19:13b.
Mwanaume anapenda kubembelezwa.
Na Mwanaume akibelezwa, anapatikana; vingenevyo akifokewa, anawaza kumkwepa na kumtoroka.
Samson alipobembelezwa na Delila, alipatikana. Waaamuzi 16:1-22.

8⃣ Wanawake wazuri sana na wenye mvuto wa kimapenzi (sexual appeal) Mithali 6:25-26.
Akikosea akautamani uzuri wake moyoni mwake ni hatari.

9⃣ Mazingira ya ulevi ni hatari sana. Lutu alipolewa alizini-Mwanzo 19:30-38.

🔟 Wanaume wenye sura nzuri (handsome) Mwanzo 39:6b-7.
Wenye vyeo (viongozi) na wafanya biashara. (Ufunuo 18:3)

NB: Wanawake ni walinzi:
Yeremia 31:22... mwanamke atamlinda mwanaume.
Mlinzi ndiye huwa wa kwanza kuwajibishwa iwapo, uharibifu ukitokea mahali.

Ni muhimu mwanamke atimize wajibu wake, na MUNGU atamtetea.
Ila mzembe na asiyesimama katika nafasi yake; atawajibika kwa MUNGU, iwapo..uharibifu ukitokea.

Lakini, hii haimaaanishi wanaume wana tiketi ya kuzini.
Ni lazima, wanaume tuombe na kupambana ili tushinde.
Mbinguni wataingia washindi tu.
Ufunuo 2:7, 11,17,26; 3:5,12,21.
Katika mambo hayo yote, tunashinda na zaidi kwa Yesu Kristo aliyekupenda. Warumi 8:37.

Hahaaaaaaaaaaaaa kazi kwenu wazinzi
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top